Wadau,
Imeripotiwa hivi karibuni kuwa uanachama wa Zanzibar kwenye shirikisho la soka barani Afrika CAF umefutwa. Tatizo langu si uhalali wa Zanzibar kuwa na vigezo vya kuwa mwanachama au la, ila vikao vilivyoipa uanachama na vilivyofuta uanachama. Kwa uelewa nilionao ni kwamba mkutano Mkuu wa CAF ndio ulioipa uanachama Zanzibar tena kwa kura za kutosha na ndio Kikao chenye maamuzi ya mwisho kuhusu soka barani Afrika, sasa iweje kamati ya utendaji ya CAF iliyokutana Morocco iifutie uanachama Zanzibar wakati Kikao cha juu kilishaamua vinginevyo? Hii ni sawasawa na mahakama ya mwanzo kutengua maamuzi ya mahakama ya wilaya.
Kama kamati kuu wamegundua kwamba Zanzibar ilipewa uanachama kimakosa, nadhani walitakiwa kuirudisha hoja hiyo kwa mkutano Mkuu wa CAF na kutoa hoja zao ndipo maamuzi yafanyike, vinginevyo naona maamuzi hayakufuata utaratibu.
Hoja kuu ina mashiko, CAF hawatoi uanachama mara mbili kwa nchi moja, vinginevyo Zanzibar ijitutumue ijitangaze ni nchi kamili umoja wa mataifa waitambue, na hilo haliwezekani kamwe.