Inaweza kuzaliwa Zanzibar mpya. Mfano wanaweza kuunda selikari yao ya Muungano wa visiwa vya Pemba na Unguja. Selikari ya Pemba na Selikari ya unguja zikishughulika na mabo yao ya ndani na Selikari ya Muungano ikishughulikia mambo ya Muungano wao.
Pia maridhiano yanaweza kufanyika kwa raia watakaoamua kubaki kwa hiari yao katika sehemu mojawapo zilizokuwa zinaunda muungano uliovunjika. Tutakapoamua kutumia Busara au Jazba kakika kuvunja muungano ndivyo vitakavyoamu yale yatakayotokea siku ya kuvunjika kwa muungano. Montenegro walipiga kura kujitoa kwenye Muungano na Serbia, Serbia kwa shingo upande wakaamua kuwaruhusu lakini hawakuchukua hatua za kuwafukuza wamontenegro waliokuwa wanaishi serbia. Sana sana Serbia ilitafuta njia nyingine ya kuimarisha mahusiano na Montenegro na si kuendeleza uhasama. Hivyo hata kwa Tanganyika na Zanzibar kuna mambo mengi tunaweza kufaidishana baada kama muungano wetu tutauvunja kwa kufuata taratibu zinazotakiwa badala ya kutumia jazba, kujenga uhasama, n.k
Nadhani Semilog umejibu kitaalamu hili. Na wapemba wanaokuwepo Unguja katika jimbo lolote lile hawawezi kushinda uwingi wa wa_Unguja waliopo katika jimbo hilo- Ndiyo maana wanashindwa Unguja. Lakini hii hali siyo nzuri Kwa nini watu wapige kura on this basis. Walioasisi mtizamo huo walikuwa na tamaa zao. Sisi kwa nini tunatumbukia huko. Ndiyo maana nasema kule Zanzibar tuachane na CUF , tuachane na CCM, tuachane na kumbukumbu za tuliowazika za ASP na Hizbu. Tuanze upya . tuanzishe vyama vyetu pale Zanzibar( ni kwa ajili ya Zanzibar tu-tupige siasa ) na tuingie katika kura kutafuta Rais na Wawakilishi.Bara hawamo na hawahusiki kwa lolote lile.
Hakuna faida yeyote ya muungano, kuna mabadiliko gani wazanzibari walio pata baada ya muungano? Na kwanini Tanzania bara hawataki kuiachia zanzibar? Muungano uvungike na tuone kama wabara hatutagombania kwenda zenji. hii yote ni staili ya CCM ya divide and rule. hawa wakiwa kitu kimoja ndio watapata mabadiliko. Yani toka Waomani walivyo ijenga zenji ni mpaka leo hakuna kilicho zidi. Hata hizo nyumba za karume mpaka leo zimewashinda.
Kwanza nawasalimu wote wapenzi wa Jamii forum na michango yao mizuri, mimi ni mpenzi sana wa Forum huwa sikosi kuwasikiliza na kusoma post zenu kila siku, ila sasa nimeamua pia kuwa miongoni mwa wachangiaji ili na wengine wasome mawazo yangu, nafikiri ni uamuzi mzuri tu.
Kwa keli swala la Nzanzibar ni gumu sana kama tunavyolichukulia, Mimi binafsi nakubakliana kabisa na mtoa mada kuwa itakuja geuga Burundi kwani , wakibaki pekee yao wapemba hawaamini kama wale wa unguja ni wenzao, wanaamini waunguja ni watu wa bara, na pemba wanaamini wao ni jamii ya mwaarabu na hawakubaliani na mapinduzi yaliyofanywa ya kumtoa sultani, hadi leo wanaamini sultani alitakiwa awepo na ndiye ndugu yao.
Kama unataka kuhakikisha hilo , Fanya utafiti kwa kukutana na wa pemba wanaoishi nje ya Tz jaribu kukaa nao na ongea nao mawazo yao na fanya hivyo kwa watu zaidi ya 10, utakuta wana mawazo yaliyo sawa. Nimekutana na wapemba zaidi ya 20 nje ya nchi, na nimeishi nao vizuri lakini inapofika kusema wao ni watanzania , basi mtabishana hadi asubuhi na hata mkiita kikao cha Watz ni nadra sana kuhudhuria, na sababu kubwa wanasema sisi siyo ndugu zao, ndugu yao ni mwaraabu. Kwa hali hiyo Muungano ukifa wataanza kuwabagua waunguja kuwa wametoka bara. na mwisho wake itakuwa kupigana kana kama Burundi, Mtusi na Mhutu. Tusiombee hayo lakini HABARI NDIYO HIYO!!!
Visiwa hivi vitaendelea kuwa sehemu ya Jamhuri!
Huo ndo ukweli!
Kama yakigunduliwa mafuta wachimbe tu kama jinsi wanavyopata pesa ya utalii hawaingiliwi!
Ila waache kusamehe watu kutolipa kodi na kisha kuanza kulalamika wanaonewa wakati kodi 50% haikusanywi!
Nimeshafanya kazi sehemu yenye wapemba na waunguja wengi, mimi(mbara) uk. Yana wanabaguana mpaka basi. Lakini waunguja wako karibu na wabara. Ukitoka eneo la kazi huko nje ndio kabisaaa, yaani ukimuona mmpemba ambaye ubaguzi wake mdogo basi ameishi unguja.
Kama unaona burundi hatari, basi ni kama wajaluo na wakikuyu....
Kwanza nawasalimu wote wapenzi wa Jamii forum na michango yao mizuri, mimi ni mpenzi sana wa Forum huwa sikosi kuwasikiliza na kusoma post zenu kila siku, ila sasa nimeamua pia kuwa miongoni mwa wachangiaji ili na wengine wasome mawazo yangu, nafikiri ni uamuzi mzuri tu.
Kwa keli swala la Nzanzibar ni gumu sana kama tunavyolichukulia, Mimi binafsi nakubakliana kabisa na mtoa mada kuwa itakuja geuga Burundi kwani , wakibaki pekee yao wapemba hawaamini kama wale wa unguja ni wenzao, wanaamini waunguja ni watu wa bara, na pemba wanaamini wao ni jamii ya mwaarabu na hawakubaliani na mapinduzi yaliyofanywa ya kumtoa sultani, hadi leo wanaamini sultani alitakiwa awepo na ndiye ndugu yao.
Kama unataka kuhakikisha hilo , Fanya utafiti kwa kukutana na wa pemba wanaoishi nje ya Tz jaribu kukaa nao na ongea nao mawazo yao na fanya hivyo kwa watu zaidi ya 10, utakuta wana mawazo yaliyo sawa. Nimekutana na wapemba zaidi ya 20 nje ya nchi, na nimeishi nao vizuri lakini inapofika kusema wao ni watanzania , basi mtabishana hadi asubuhi na hata mkiita kikao cha Watz ni nadra sana kuhudhuria, na sababu kubwa wanasema sisi siyo ndugu zao, ndugu yao ni mwaraabu. Kwa hali hiyo Muungano ukifa wataanza kuwabagua waunguja kuwa wametoka bara. na mwisho wake itakuwa kupigana kana kama Burundi, Mtusi na Mhutu. Tusiombee hayo lakini HABARI NDIYO HIYO!!!
Hali ya kisiasa ya zanzibar ilivyo sasa hivi ni kama burundi au rwanda.
Zanzibar hakuna upinzani wa kisiasa bali kuna ukabila. Waunguja wanapigia kura ccm na wapemba cuf.
Kwa mantiki hiyo ninaamini kwamba endapo muungano utavunjika na ikarudi kuwa tanganyika na zanzibar, miezi mitatu ya mwanzo itakuwa ni furaha kwa wazanzibar kwa ajili wamekua na nchi yao wenyewe, halafu machafuko yataanza pale uchaguzi wa kumteua rais wa zanzibar utakapoanza. Wapemba watapigia kura cuf na waunguja ccm(asp) na hapo ndio zanzibar itakapopasuka na unguja kuwa nchi na pemba kuwa nchi na rais wake sshamad. Wapemba hatakubali rais awe muunguja kwa ajili imekua hivyo siku nyingi sana na waunguja wanaamini kwamba wapemba ni wabaguzi watawabagua sana.
mambo yote haya yatatokea katika kipindi cha mwaka mmoja.
fact: Uk kuna wazanzibari wengi lakini wamegawanyika katika makundi mawili wapemba na waunguja. Waunguja wapo karibu na watu wa bara na wapemba wako wenyewe. Pamoja na kuja ulaya bado wameshidwa kuwa ndugu. Kama wakikuyu na wajaluo uk
Athari za kuvunjika kwa muungano
1.wa bara waliokuwa zanzibar wataambiwa warudi kwao na wengine hata kupoteza maisha yao. (hawako wengi)
2. Wapemba ambao wanamaduka bara itabidi wayafunge na warudi kwao, sijui pemba ilivyokuwa ndogo watamuuzia nani vitu.
3.wazazibari wenye magorofa kariakoo itabidi wayaache na warudi kwao. Hata mzee mwinyi itabidi aondoke aliache lile gorofa lake msasani na white sands hotel.
4. Kwa sisi tuliooa zanzibar itabidi wake/waume zetu warudi zanzibar na watoto wabakie bara (kitu kibaya sana hichi).
5. Wakati mamboa yote haya ya kiendelea wananchi wakitaabika viongozi watakua wanagawana madaraka. Je wazanzibari mmefikiria au ni kufuata mkumbo wa viongozi
mkoa wa kinondoni una watu zaidi ya zanzibar nzima.
Solution: Kuwa na serikali moja rais mmoja na pemba na unguja kuwa mikoa yenye ma mayor ambao watapigiwa kura na wananchi.