Zanzibar and Tanganyika vie over oil reserves

simplemind

JF-Expert Member
Apr 10, 2009
16,418
9,206
Zanzibar and Tanzania vie over oil reserves

The most recent involves the United Republic of Tanzania and the semi-autonomous region of Zanzibar.

Despite a strong desire to reap the rewards from oil and gas within its boundaries, investors in the region are hoping that the two governments will realise that it is better to share revenue than risk deterring investment.

Against a backdrop of recent disputed matters involving Kenya and Somalia, and Ghana and Ivory Coast, which some speculate will start a plethora of maritime boundary disputes in Africa, hopes for Tanzania rest on a referendum for a new constitution.

Under the current constitution, formulated following the union between Tanganyika (mainland) and Zanzibar in 1964, the government of Tanzania has control over “Union matters” while the government of Zanzibar is left to control matters which solely affect Zanzibar.

Crucially, petroleum exploration is deemed to be a Union matter and, as a result of the potential volumes of hydrocarbons in and around Zanzibar, this matter has added impetus to calls for a greater level of autonomy for Zanzibar.

The principle reason for this has been Zanzibar’s dissatisfaction with the production sharing arrangements administered and negotiated by the state-owned Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC), particularly regarding the revenue sharing mechanism.

In response, the government of Zanzibar has formed its own national oil company, the Directorate of Petroleum, through which it seeks to negotiate its own terms and collect its own revenue. Though not officially recognised by the government of Tanzania, the Directorate of Petroleum has created uncertainty in the minds of exploration companies, resulting in a halt of exploration activity since 2004.

This has led the government of Zanzibar to demand that petroleum resources should not be classified as a Union matter within the constitution, but rather that Zanzibar’s resources should be under the jurisdiction of the government of Zanzibar.

The proposal sets out that the regulation of oil and gas exploration (and the negotiation of any production sharing arrangements) should be carried out by either of the two proposed regional governments – potentially paving the way for the recognition of two separate national oil companies. The referendum on the new proposed constitution, which was scheduled for April 2015, did not take place and has been put on hold indefinitely.

The situation in relation to offshore blocks is even less clear cut. Given most of the probable oil reserves are offshore, maritime boundary disputes may arise if further clarification is not provided..

The need to establish a maritime boundary
If Tanzania does eventually approve a new constitution, it is quite conceivable that the mainland and Zanzibar have to debate the need for a maritime boundary. If they fail to reach an agreement, there may be a formal adjudication of the maritime boundary in accordance with the UN Convention on the Laws of the Sea.

Given the slowdown in exploration work in Zanzibar due to unresolved issues, an agreement on a maritime boundary would be beneficial for Tanzania as a whole.

The way forward
It is expected that the mainland and Zanzibar will agree a boundary treaty. However Tanzania is already engaged in a similar debate with Malawi, where gas fields lying under Lake Malawi have led to tensions between the government of Tanzania and the government of Malawi.

At a time when East Africa’s prospects of becoming a major participant in the global gas industry are being threatened by falling oil prices and legislative deficiencies, a new constitution in Tanzania to settle the matter would offer positive signals to the oil and gas industry. However constitutional reform is only the first step in clarifying Zanzibar’s hydrocarbon regime.

Source: insideafricalaw
 
MAKUBALIANO ya mkataba wa awali (MoU), uliosainiwa hivi karibuni baina ya Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dk Ali Mohamed Shein, na kampuni ya kimataifa ya
mafuta ya Shell unaohusu utafutaji na hatimaye uchimbaji wa mafuta, umeelezwa kuwa ni
mkataba ‘feki’ na usiokuwa na uhalali wowote kisheria.
Magwiji wa sheria na mikataba nchini, Profesa Issa Shivji na Dk Rugemeleza Nshala, kwa
nyakati tofauti, wameliambia gazeti hili kuwa hicho kinachodaiwa kusainiwa na Dk Shein na
kampuni hiyo ya Shell, hakipo kisheria kwa maelezo kwamba mafuta na gesi asilia ni
mambo yaliyo chini ya Muungano, na kwa hiyo mwenye mamlaka ya kusaini mkataba wa
aina hiyo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, ni waziri mwenye dhamana kuhusu masuala
ya nishati.
Katika toleo la wiki iliyopita, gazeti hili lilibeba habari kuu iliyokuwa ikielezea namna Dk
Shein alivyoingia makubaliano ya awali (MoU) na kampuni kubwa ya kimataifa
inayojishughulisha na biashara ya nishati ya mafuta na gesi asilia, Shell, wakati akiwa
katika ziara yake ya kiserikali nchini Uholanzi, Agosti mwaka huu.
Katika mkataba huo wa makubaliano ya awali, SMZ imeipatia kampuni hiyo ya Shell idhini
ya kutafiti na hatimaye kuchimba mafuta katika vitalu vinne, vilivyopo Zanzibar,
vilivyopewa majina ya Block 9,10,11 na 12.
Akizungumzia hatua hiyo wiki iliyopita akiwa mjini Kilwa Masoko kwa ajili ya kutoa mafunzo
yanayohusiana na masuala ya mafuta na gesi kwa wanahabari nchini, yaliyoandaliwa na
Baraza la Habari Tanzania (MCT), Profesa Shivji, alisema Dk Shein hana mamlaka yoyote
hadi sasa ya kisheria kusaini mkataba wowote unaohusiana na masuala ya mafuta na gesi
ndani ya eneo la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Alisema mafuta na gesi ni mambo ya Muungano, na kwa hiyo mamlaka pekee yenye uhalali
wa kisheria kusaini mkataba wowote unaohusiana na jambo hilo, ni Serikali ya Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania.
Aidha, Profesa Shivji aliwataka Watanzania kuwapuuza wote wanaodai kwamba masuala ya
mafuta na gesi asilia viliingizwa kinyemela katika mambo yote ya Muungano, akisisitiza
kwamba maliasili hiyo iliongezwa kwenye mambo ya Muungano mwaka 1968 wakati wa
utawala wa Mzee Abeid Amani Karume.
“Masuala ya mafuta na gesi yaliongezwa kwenye mambo ya Muungano na Mzee Karume
mwenyewe mwaka 1968. Zitafuteni Hansard (taarifa mazungumzo yaliyofanyika ndani ya
Bunge), zipo. Hao wanaopiga propaganda kwamba mambo hayo yaliingizwa kinyemela
kwenye mambo ya Muungano ni watu wa kupuuzwa,” alisema Profesa Shivji.
Kwa upande wake, Dk Nshala alisema kwa kusaini
makubaliano hayo, si tu kwamba Dk Shein amevunja Katiba, bali hata kampuni yenyewe ya
Shell iliyosaini mkataba huo, imesaini mkataba kanyaboya (feki) kutokana na kile
alichosema kampuni hiyo imeingia makubaliano na mtu asiyehusika kwa mujibu wa sheria
ya sasa ya madini, mafuta na gesi.
“Mwenye mamlaka ya kisheria kusaini mkataba wowote unaohusu nishati na madini, kwa
mujibu wa Katiba yetu, kwa niaba ya Serikali yetu, ni Waziri wa Nishati na Madini. Suala la
mafuta na gesi asilia viko chini ya Muungano, Dk Shein hana uhalali wowote wa kusaini
mkataba wa mafuta, gesi wala madini…unajua kuna watu wanataka kutumia kipindi hiki
ambacho tuko kwenye mchakato wa kuandika Katiba Mpya kuvuruga Muungano,” anasema
Dk Nshala ambaye amebobea katika masuala ya mikataba ya madini, mafuta na gesi.
Raia Mwema linafahamu kwamba ingawa MoU inaonyesha kwamba walioingia makubaliano
ni Shein na Mtendaji Mkuu wa Shell, Peter Voser, aliyesaini mkataba huo kwa niaba ya
Shein ni Waziri wa Nishati wa SMZ, Ramadhan Abdallah Shaaban.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Katiba na maelezo ya Prof. Shivji na Dk. Nshalla, aliyepaswa
kusaini makubaliano kama hayo kwa sasa ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter
Muhongo.
Soma zaidi kuhusu:
Tufuatilie mtandaoni:
Endelea Kuhabarika
Gesi, mafuta yaivuruga Katiba
Tunahitaji Mamlaka ya Gesi na Mafuta – Zitto
Mpango wa TEITI una manufaa katika gesi na mafuta?
Nini gesi na mafuta?
Maoni ya Wasomaji
Wataalamu kingeni ndimi zenu
Permalink Submitted by Msomaji wetu (not verified) on Sun, 2013-10-13 17:56.
Wataalamu kingeni ndimi zenu wakati mambo yenye kusokota Taifa yanapotukabili.
Suala la gesi na mafuta hata kama kisheria ni la Muungano basi haisaidii kwa wakati
huu kujaribu kuchukua msimamo ambao ni wazi kabisa unahifadhi matakwa ya upande
mmoja na hasa ilivyokuwa nyinyi nyote wawili mnatokea upande huo huo mnaonufaika
na mfumo uliopo. Nasema hivyo kwa sababu haimkiniki kuwa hamtambui mabishano
yaliyopo ya pande hizo mbili za Muungano. Tunajua lolote linalotaka kufanywa na
Zanzibar lazima lipitie Dodoma. Mambo ya fedha ndio kabisa. Nono linabakia huko huko
na vijisenti ndio hupewa Zanzibar. Hivyo kweli mnaamini kwamba wanasheria wote wa
Zanzibar ni mbumbumbu namna hiyo? Kutoa maelezo reja reja kwa kujibanzia sheria
inaeleza hivi na vile ijapokuwa jumba lote la sheria za Muungano tangu huko
tunakotoka zina ghilba. Kusema kwamba tangu enzi za mzee Karume jambo hili
limeshatiwa katika Muungano kwa hivyo halina mjadala mmpepotea njia. Pitieni
Hansard za Baraza la Wawakilishi muelimike na mtazamo wa Wazanzibari. Sheria bila
haki haitodumu
 
Tatizo ambalo huyo Shivji mwenyewe amejikanganya ni uhalali wa huo muungano wenyewe ambao ni feki.

NJAA INAMSUMBUA MASIKINI SHIVJI

Makala

Ni utatanishi wa rasimu au wa Shivji binafsi?
Mwandishi Wetu
Toleo la 302
10 Jul 2013

HIVI karibuni Prof. Issa Shivji alitoa mhadhara wa kisomi juu ya rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Warioba, kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maoni.

Mhadhara huo alioutoa Juni 21, 2013 kwenye ukumbi wa Nkrumah Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam katika kuaga uongozi wa Kigoda cha Taaluma cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mhadhara huo ulifuatiliwa kwa karibu na wananchi wengi kupitia vyombo vya habari kutokana na umaarufu na umahiri wa mtoa mada katika medani ya usomi wa sheria na mambo ya katiba nchini.

Katika mhadhara huo alijadili mambo mengi lakini sasa nitajikita kwenye maoni yake kuhusu kile alichokiita kwa usahihi kabisa kuwa ni moyo wa Katiba, yaani Muungano. Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa kwa kiwango kikubwa maoni yake kuhusu Muungano yanaonekana kuwachanganya wananchi wengi hasa wale ambao wamekuwa wakifuatilia maoni yake kuhusu Muungano katika mawasilisho yake mbalimbali.

Kwa kiwango kikubwa maoni ya Prof. Shivji yamekuwa na utatanishi na mkinzano yenyewe kwa yenyewe au baina ya wakati mmoja na wakati mwingine.

Katika mada yake, Shivji anasema kuwa muundo wa shirikisho uliopendekezwa na Tume hauwezi kukidhi mahitaji ya pande zote mbili bila hatari ya kuvunja Muungano. Badala yake amependekeza muundo mbadala wa serikali mbili.

Kwa maoni hayo, Shivji anapingana na maoni yake aliyoyatoa mwaka 1990 katika kitabu chake, “The Legal Foundations Of The Union in Tanzania’s Union and Zanzibar Constitutions.” Katika kitabu hicho Prof. Shivji anasema

“…..The union of Tanganyika and Zanzibar was founded on strong and time-honoured principles of federalism……the legal foundations of the Union are to be found within the four walls of the Acts of Union which ratified and approved the treaty called the Articles of Union….”(Shivji,1990, Uk.90)

Tafsiri yake ni kuwa, Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ulianzishwa kwa misingi imara ya shirikisho na misingi hiyo inaonekana wazi kwenye Hati ya Muungano. Katika kitabu hicho Shivji alionyesha kuwa muundo wa sasa wa serikali mbili uko kinyume na Hati ya Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar ya Mwaka 1964.

Kwa maana hiyo, Shivji alitakiwa awaambie Watanzania kwa nini amebadilisha mawazo au la angeipongeza Tume kwa kuurudisha Muungano katika asili yake kwa kadiri ya maelezo yake ya awali na labda angetoa maoni ya namna ya kuboresha muundo huo.

Utata katika maoni ya Shivji kuhusu Muungano yalionekana tena mwaka 2008 kwenye kitabu chake Pan-Africanism or Pragmatism. Katika kitabu hicho, anatilia shaka uhalali wa Muungano kisheria na kisiasa.

Kwenye kitabu hiki anasema kuwa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha uhalali wa kisiasa na kisheria wa kuwepo kwa Muungano. Hapa, Prof. Shivji aliamua kupingana na ushahidi alioutumia yeye mwenyewe mwaka 1990 ikiwamo Hati ya Muungano ambayo alibainisha kuwa ndiyo msingi wa Muungano.

Kama ilivyosemwa hapo juu, kwenye mhadhara wake wa kuchambua rasimu ya Katiba mpya alioutoa Juni 21, 2013 kwenye ukumbi wa Nkrumah, Prof. Shivji anapendekeza muundo mbadala wenye “dola kamili mbili, la Zanzibar na Muungano” (Uk. 40).

Kama alivyosema mwenyewe kwenye mhadhara huo, Prof. Shivji alipendekeza muundo huo mbadala kwa Baraza la wawakilishi-Zanzibar, Januari 17 2013. Aliliambia Baraza la Wawakilishi kuwa anapendekeza Muungano wa Dola Mbili Huru, yaani nchi huru na dola zenye mamlaka kamili “sovereign state” mbili.

Mapendekezo ya Prof. Shivji, ya kuwa na Muungano wa nchi mbili huru (sovereign states) umejaa utata kwani haiwezekani ukawa na “two sovereign states in one.” Hapa ni muhimu, japo kwa ufupi tuelewe dola ni nini. Kwa mujibu wa Mkataba wa Montevideo juu ya Haki na Wajibu wa Dola (Montevideo Convention on Rights and Duties of States) wa mwaka 1933, viashiria vya dola ni pamoja na kuwa na raia, mipaka inayotambuliwa kimataifa, serikali yenye mamlaka kuu ndani ya nchi na uwezo wa kushughulika na masuala ya kimataifa. Katika muundo uliopo dola ni moja tu. Kwa maana hiyo, pande mbili za Muungano haziwezi kuwa na raia wao bali wanaweza kuwa na wakazi tu.

Hata katika muundo unaopendekezwa na Tume ya Warioba, dola ni moja tu chini ya serikali ya Jamhuri ya Muungano. Serikali za washirika wanaweza tu kuwa na mamlaka yao lakini si ya kidola. Sheria za Kimataifa ikiwemo Mkataba wa Montevideo zinasema kuwa dola iliyo kwenye muundo wa shirikisho itatambulika kama moja kwenye macho ya sheria za kimataifa.

Hivyo, nchi kama Marekani, Uswisi, Ujerumani na kwingineko pamoja na kuwa zinafuata muundo wa shirikisho, katika jamii ya kimataifa inachukuliwa kuwa dola moja. Kwa kufafanua zaidi, ni kuwa haiwezekani sehemu moja ya nchi ikaingia kwenye vita bila sehemu nyigine kuhusika kwa kuwa vita inahusu dola kwa hiyo eneo moja la nchi likivamiwa inahesabika kuwa nchi yote imevamiwa.

Hivyo, ina maana kuwa, pendekezo la Shivji la kuwa na Muungano wa Dola Mbili Huru litahitaji kwanza kuvunja Muungano ili kila upande uwe na madaraka kamili halafu baada ya hapo ndiyo kuwe na Muungano kwa kuwa haiwezekani kuwa na dola mbili huru au hata zaidi kabla ya kuivunja dola iliyopo.

Kama alivyoeleza, Prof. Shivji kwenye Baraza la Wawakilishi, baada ya hapo, pande mbili zitaamua kupunguza ‘soveregnity’ kwa maslahi yao ya kijumla. Hapa ina maana kuwa muundo anaoupendekeza Shivji hauna tofauti na muundo wa mkataba unaopendekezwa na watu kama Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad hata kama maneno wanayotumia yanaweza kuwa tofauti.

Utata huu unaonekana ni mwendelezo au kufanyia kazi maoni aliyoyatoa kwenye kitabu cha Pan-Africanism or Pragmatism. Kwa kuwa kama Muungano hauna uhalali basi kuwe na nchi mbili huru ambazo zitaamua kushirikiana kadiri watakavyotaka.

Pia, izingatiwe kuwa katika muundo wa Muungano anaoupendekeza ambao aliuweka kimchoro kwenye mawasilisho yake kwa Baraza la Wawakilishi, Prof.Shivji, haonyeshi kokote dola itakayokuwa inashughulikia masuala ya Tanzania Bara/Tanganyika. Hii inaweza kuonyesha kuwa kwake Dola la Muungano ndiyo Dola la Tanzania Bara.

Kutokana na utata na mkinzano wa hoja za Prof. Shivji kuhusu Muungano, ambao kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa Muungano ndiyo “moyo wa katiba” ni wazi kuwa hayuko wazi na kwa kweli kuna utatanishi mwingi kuhusu mawazo yake juu ya suala hili nyeti kwa mustakabali wa nchi yetu.

Prof. Shivji, kama msomi mwenye ushawishi mkubwa katika nchi yetu maoni yake hayapswi kuwa na utata, maana yanawachanganya wananchi. Aidha, Profesa kama walivyo raia wengine wana haki ya kutoa maoni yao lakini, ni muhimu kuwa wazi ni nini wanakitaka, Profesa, ni Muungano upi unaoutaka?

Mwandishi John Missanga, amejitambulisha kama msomaji wa Raia Mwema na anapatikana kupitia baruapepe; missanga73@gmail.com
- See more at: Raia Mwema - Ni utatanishi wa rasimu au wa Shivji binafsi?
 
Back
Top Bottom