Scott alichukua usukani baada ya aliyekuwa Rais Michael Sata kufariki
Chama tawala nchini Zambia (PF) kimemtimua kaimu rais wa nchi hiyo Guys Scott kutoka chamani na kuvunja utaratibu wa katiba. Taarifa hii ni kwa mujibu wa msemaji wa chama hicho.
''Amekuwa akiwaajiri na kuwafuta watu kazi ovyo na pia bila ya kushauriana na kamati kuu ya chama,'' amesema Malozo Sichone. Bwana Scott, ambaye licha ya hatua hiyo ataendelea kuwa mwanachama wa chama hicho, ataendelea kuhudumu kama kaimu rais hadi uchaguzi utakapofanyika tarehe 20 Januari.
Scott aliteuliwa kuwa kaimu rais kufuatia kifo cha hayati Rais Michael Sata aliyefariki mwezi jana. Mia
Chanzo:BBC
CHAMA CHAMFUKUZA RAIS: Kaimu rais wa Zambia, Guy Scott leo atimuliwa kwenye chama chake cha Patriotic Front kwa 'kutoheshimu katiba', Uongozi wa Chama wasema.