Kwanza nashukuru kwa mada hii si mbaya kukumbuka ulikotoka na kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyokuvusha,pole sana kwa kumpoteza baba yako Bwana ametoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.Nami sitaisahau tarehe 11.02.2012 saa11 nikiwa KCMC nilimpoteza Baba yangu mpenzi,nikishuhudia kwa macho yangu jinsi baba yangu akimaliza safari ya mwisho kwa mateso makubwa kutokana na ugonjwa ulokuwa unamsumbua,dah! Iliniuma sana sikuwahi kuwaza ingenitokea hivyo tena mikononi mwangu, niliumia zaidi kwan nikitafakar sijarudisha bado matunda kwake kwa kunilea,yaan ndo naanza tu safar ya mafanikio ndo na yy anatoweka,iliniuma zaid siku ya harus yang mwez wa nane nilipokuwa simuon.Lakini ktk yote hayo namshukuru Mungu amenipa amani ya ajabu sijawahi kuiona maishani mwangu,sina uchungu tena moyoni mwangu japokkuwa kila siku namkumbuka lakini si ktk hali ya uchungu,leo asubuhi nikiwa nasal nikajikuta nakumbuka ktk meng Mungu aliyonishindia nikajikuta namshukuru Mungu sana na Kusema HAIKUWA JAMBO RAHISI, kwanini nasema hivyo mie kwetu ni kifunga mimba na ktk watoto wote peke yangu ndo niliyekubal shule na kufika mahali angalau baba alipokuwa anataman wanawe tufike kutokana na hilo liliniweka karibu sana na baba yangu.Mwisho nasema HAIKUWA JAMBO RAHISI kufikia hapa tulipo wana JF ila ni kwa NEEMA YA MUNGU TU,Poleni wote mlofikwa na mabaya AMANI YA MUNGU IPITAYO FAHAMU ZOTE IWAJAZE MIOYO YENU,Mungu atulinde tumalize vyema na tuanze mwaka vyema na kwa upya zaidi.Mungu awabariki wote.