Heshima kwenu wana JF:
Nimekuwa nikijiuliza sijui ni wapi tunakoelekea, sijui ni mwisho wa dunia!? au ndio maendeleo!?
Yaani sielewi kabisa, Sijui ni malezi baadhi ya watu!?
Nimeonelea neweze kutumia jukwaa hili la MMU (Mahusioano, Mapenzi na Urafiki) Kwa sababu hili jambo linahusika na uhusiano wa kijamii.
Mambo yanayo nitatiza kabisa ni yafuatayo:-
1. Watu wamekuwa wapinzani wa kila jambo
Yaani kumekuwa hakuna utaratibu wowote kabisa. Yaani utakuta watu wanapinga kila jambo ndani yamakundi ya kidini, nchi, au kundi fulani. Yaani utakuta watu wengi sikuhizi ni ma much know vibaya. Yaani utakuta mtu anapinga tu bila hata sababu, hata kama anasababu haoneshi njia iliyo sahihi.
Sijui ndugu tunaelekea wapi kumekuwa hakuna utaratibu kabisa.
2. Watu kulalamika lalamika kila wakati
Siku hizi watu umiza kichwa yaani kila wakati wanalalamika tu, kujihurumia kwingiii, yaani mpaka mimi ninakereka kabisa. Utakuta kijana ananguvu na anauwezo yaani kila wakati analaumu tu hataki kufanya initiative. Kwa mfano tu yaani watu kwenye mitaa yao wanataka serikali ije ifyeke nyasi zilizo vichochoroni. Yaani utakuta mijitu inanguvu ina lalamika oh serikali haitaki kutufanyia hili wala lile.
Mfano mwingine kwa wenyeji wa dar maeneo ya masaki karibu na Sea Cliff village pale barabarani kuna bonge la shimo vua ikinyesha maji yana jaa. Nina shangaa hapo kuna majumba mazuri mazuri na bahari ipo karibu kweli yaani kuchangishana na kukodi gari likaleta mchanga na kufukia shimo wameshindwa!?!?
Utakuta mtu mzima kabisa amepanga vitofari kwenda nyumbani kwake ndani ya maji yaani akitoka amevaa vizuri na utakuta anajiita pedeshee, nyumba nzuri lakini mazigira sasa mabooovu. Hivi tatizo nielimu ya mazingira au ujinga tu!!?
Utakuta kijana ananguvu kabisa hataki kufanya kazi za nguvu wakati kuna issue nyingi tu za kufanya, kunakubeba zege, kujenga mabarabara nk. Yaani kijana anataka kazi laini laini za kubonyeza komputa. Kila kukicha analaumu serikali, Hafanyi chochote
Ina boa sanaaa.
Nchi yetu ina ardhi kubwa kweli yaani vijana wanaweza wakaungana na kuenda kufyeka pori wakalima na kujipatia kipato. Lakini kila kukicha wanalaumu, wanalalamika
Kazi ndio msingi wa maendeleo.
Jitume fanyakazi Mungu atabariki kazi ya mikono yako.