Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,664
- 8,278
Uchezaji mzuri uambatane na matokeo chanya. Ikiwa matokeo ni hasi, binafsi sioni mantiki ya kuwasifia kuwa timu inacheza vizuri.Yanga msivunjike mioyo, uaminini mradi mliyoanza kuujenga, inatakiwa mkubali bado ni changa inaendelea kukua.
Timu inacheza vizuri cha msingi ni kuboresha sehemu ndogondogo zilizosalia hasa ulinzi.
Ni mambo gani yafanyike ili timu ya Yanga ifike mbali? Unaposema "wekeni nguvu", unamaanisha nini?Wekeni nguvu kwenye Michuano ya Shirikisho huenda huko mkafika mbali.
Msikubali kukatishwa tamaa, endeleeni kujaribu tena na tena, keep pushing.
Waswahili wanasema "Jitihada hazimtupi mkulima".
Hakuna kipindi ambacho mashabiki wa Yanga mnapaswa kuwa karibu na timu kama kipindi hiki.
Mtatupiwa uchafu wa kila aina, mkikubali kwenda na upepo mtaivuruga timu ambayo imeanza kuonesha mwanga.
Kukata tamaa ni dhambi. Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi.
Muelewe giza linapozidi ujue pamekaribia kupambazuka.
Yanga, Trust the process. [emoji119]