Ni nani hasa anayeruhusu uhujumu uchumu wa Klabu ya Yanga SC kwenye suala zima la jezi.?
Ni kiongozi yupi wa Yanga SC asiyejua kuwa suala la jezi lina maslahi mapana kwa klabu.?
Nimekuwa nikifuatilia hizi jezi Mpya za Yanga ambazo zinasemekama zinaenda kutumia msimu ujao wa 2017/18. Hizi jezi zinauzwa kama njugu, cha ajabu zaidi ni kwamba Klabu haipati mgawo wowote ule kutoka na na mauzo ya Jezi hizi.
Ni tofauti sana wanavyofanya klabu kubwa nyinginezo ambapo percentage ya mauzo ya jezi ya klabu husika yanarudi klabuni. Hivyo kuifanya klabu kuwa na chanzo cha ziada cha mapato.
Ebu Fikiria: Jezi moja tu inauzwa kwa Tsh 20,000/= ambapo hakuna hata senti 5 inayoingia klabuni. Ni biashara gani hii wanayoifanya YANGA SC?
Bila shaka kuna kiongozi mule ndani anahusika moja kwa moja na dili hili ambapo kwa story za chini ya kapeti zinasema yeye pekee anavuta ka'mkwanja kwa kuidhinisha utengenezaji wa hizi jezi na huyo mzalishaji.
Nataka viongozi wangu watambue kuwa Yanga ni Brand kubwa sana, iweje suala la jezi linamnufaisha mtu binafsi na sio klabu. Na hapo hapo tunalazimika wanachama kuchangia klabu inapoonekana hakuna pesa za kutosha kuendesha klabu.
Wana Akili ya kutwaa mataji...nyie kazi kufanya ibada..mmekuwa BAKWATAHivi ni tangia wana Yanga walikuwa na ' akili ' za Kimaendeleo?
itabidi Yanga labda mfanye ule u-Msama. unamkumbuka Msama na kazi za wasanii??Ni nani hasa anayeruhusu uhujumu uchumu wa Klabu ya Yanga SC kwenye suala zima la jezi.?
Ni kiongozi yupi wa Yanga SC asiyejua kuwa suala la jezi lina maslahi mapana kwa klabu.?
Nimekuwa nikifuatilia hizi jezi Mpya za Yanga ambazo zinasemekama zinaenda kutumia msimu ujao wa 2017/18. Hizi jezi zinauzwa kama njugu, cha ajabu zaidi ni kwamba Klabu haipati mgawo wowote ule kutoka na na mauzo ya Jezi hizi.
Ni tofauti sana wanavyofanya klabu kubwa nyinginezo ambapo percentage ya mauzo ya jezi ya klabu husika yanarudi klabuni. Hivyo kuifanya klabu kuwa na chanzo cha ziada cha mapato.
Ebu Fikiria: Jezi moja tu inauzwa kwa Tsh 20,000/= ambapo hakuna hata senti 5 inayoingia klabuni. Ni biashara gani hii wanayoifanya YANGA SC?
Bila shaka kuna kiongozi mule ndani anahusika moja kwa moja na dili hili ambapo kwa story za chini ya kapeti zinasema yeye pekee anavuta ka'mkwanja kwa kuidhinisha utengenezaji wa hizi jezi na huyo mzalishaji.
Nataka viongozi wangu watambue kuwa Yanga ni Brand kubwa sana, iweje suala la jezi linamnufaisha mtu binafsi na sio klabu. Na hapo hapo tunalazimika wanachama kuchangia klabu inapoonekana hakuna pesa za kutosha kuendesha klabu.
Yaani Haya maviongozi ni ziro kabisa.Mfumo wa uendeshaji wa mpira nchi hii ni wa ajabu sana. Timu hizi zinalalamika ukata wakati biashara iliyo wazi kama hii inafanywa bila kunufaisha klabu. Mashabiki na wanazi wa hizi timu wabadilike na kuleta shinikizo kubwa kwa viongozi ambao inaonekana wana maslahi na magumashi yanayoendelea.
Simba walijaribu na kuonyesha mwanga kidogo lkn sasa hivi haijulikani wameishia wapi. Kwenye mikutano sijui kama taarifa za mapato zinaonyesha mauzo ya jezi yameleta sh ngapi na kuna mkakati gani wa kuboresha
UhlSports ndio wanatengeneza hizo jezi zilizopo Kariakoo ?Sikuwahi ona Uhlsports wakifanya mauzo ya jezi za Wateja wao....
Labda utaratibu upi unao uzungumzia wewe.
Hata kukaa kimya ni busara pia kuliko kuweka pumba hati uonekane nawe umechangia.Hivi ni tangia wana Yanga walikuwa na ' akili ' za Kimaendeleo?
Mla pupa hadiriki kula tamu. Sahihisha sentensi yako kwanza ili ilete maana kabla haijabainika kwamba hilo unalowakusudia Wanayanga kwako limezidi maradufu.Hivi ni tangia wana Yanga walikuwa na ' akili ' za Kimaendeleo?