Yanga bila Tshishimbi tatizo kubwa mbele ya Simba

Affet

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
1,189
1,663
Mimi ni mpenzi kindakindaki wa Yanga nimefuatilia mara kadhaa tukicheza bila Papy tunavyohaha kupata matokeo.

Yanga inatulia sana ikiwa na Tshishimbi; dimba la chini akina Makame, Fey na wengineo. Sita yao sijui wanachezaje, timu haipush kabisa kwenda juu kwa mtu unayeangalia mpira kiufundi bila ushabiki. Kwa timu kama Simba yenye viungo wengi, kama pale kati utaingia kwa kuungaunga ni dhahama.

Najua wapo Yanga watakaoniita mbumbumbu kwa kuonesha kwangu wasiwasi mechi zote mbili zilizopita Simba alipata tabu sana na ile triangle ya Tshishimbi. Ndiyo, Balama na hata game hii kama tunakuja na hii triangle, wasiwasi sina ila bahati mbaya Balama confirmed hatakuwepo na hao wawili nao kizungumkuti. Hapo napata mashaka kidogo. Tuna viungo wengi tunaweza tengeneza triangle nyingine; cha msingi Papy tu awepo.

Niyo na Balama sio ishu sana. Kuna Makame, Fey, Banka, Kaseke naye yupo kwenye form japo nao wana chochoro upande wa kulia kule. Yule shamte si wa kumzuia Morrison au Ditram, tutafaidika sana na ule upande tukiutumia vizuri.

Yote kwa yote, tusubiri tarehe 12 tutajua nani anaanza nani hayupo. Bado tuna siku 3 zinatosha mchezaji ku-recover!

IMG-20180217-WA0017.jpg
 
Wanaitwa Wekundu Wa Msimbazi, Simba, Mnyama, Wanalunyasi, Taifa Kubwa, Wazee Wa Kidedea, Wakimataifa, Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa, Wazee Wa Vuvuzela.

Timu Inayocheza Soccer Lakiwango Kilichothibitishwa Na Shirikisho La Soka Africa CAF. Kiukweli Raha Inatunyemelea, maana Kipigo Tutachotoa Ndo Kitawafumbua Macho Kwamba Pale Utopolon Hakuna Timu.
 
Ninakuunga Mkono kabisa, sio Papy tu ila wawepo Papy Tshishimbi na Niyonzima.
 
Wanaitwa Wekundu Wa Msimbazi, Simba, Mnyama, Wanalunyasi, Taifa Kubwa, Wazee Wa Kidedea, Wakimataifa, Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa, Wazee Wa Vuvuzela.

Timu Inayocheza Soccer Lakiwango Kilichothibitishwa Na Shirikisho La Soka Africa CAF. Kiukweli Raha Inatunyemelea, maana Kipigo Tutachotoa Ndo Kitawafumbua Macho Kwamba Pale Utopolon Hakuna Timu.
Haaaaaahaaaaa mlisema hvhv kabla ya ile mbilimbili baada ya ile mkatuuliza tulipataje sare? Tukawanyiosha moja bila Safari hii mmekuja na kauli nyengine yaani mikia sijui tuwafanye nini ili muache midomo!
 
Wanaitwa Wekundu Wa Msimbazi, Simba, Mnyama, Wanalunyasi, Taifa Kubwa, Wazee Wa Kidedea, Wakimataifa, Mwana Kulitaka Mwana Kulipewa, Wazee Wa Vuvuzela.

Timu Inayocheza Soccer Lakiwango Kilichothibitishwa Na Shirikisho La Soka Africa CAF. Kiukweli Raha Inatunyemelea, maana Kipigo Tutachotoa Ndo Kitawafumbua Macho Kwamba Pale Utopolon Hakuna Timu.
😆😆😆😆😆
 
Back
Top Bottom