Maneno haya niliambiwaga na marehemu bibi yangu,
Mwanamke usiwe malaya kutembea na wanaume hovyo, sio sifa na pia usishindane na mumeo eti yeye akitoka kuchepuka na wewe unachepuka , wanaume hatuwawezi hawa hawana haya wewe toka umekuwa na mahusiano na wanaume, si unaona ukiingia nae ndani hata kwa mara ya kwanza hakujui humjui wa kwanza yeye kuvua nguo na kuzitundika kwenye msumari.
Hawana haya mbele ya wanawake , usishindane na mumeo pindi utakapoolewa ye mchi wewe ni kinu sasa utambue kinu ndio kinapata maumivu wakati wa kutwanga utachoka bure mjukuu wangu.
Yeye akifanya mambo mabaya sali piga goti kwa Mungu muombe kula vizuri penda familia yako, vaa vizuri.