Mimi ilishawahi kunikuta aisee, alafu mtu mwenyewe alikuwa mrembo sana, alikuja ofisini kwa shida yake, nikamsaidia, akanishukuru. Kesho yake akaja tena japo ishu haikuwa serious kivile, akasema nimekuja kukupa hi tu napita, nikafanya kosa la kupiga story mbili tatu, nikawa nimeharibu. Kesho yake nikaona friend request fb, nikakubali hapo nikafanya kosa la pili, akaja inbox kuniomba namba nikampa, ikawa kosa la tatu, kila siku, asubuhi, "baby umekunywa chai? umekula nini?" Mchana hivyo hivyo baby umekula lakini? wahi ukale bana kazi haziishi. Jioni baby umekula nini leo? Saa nne baby umeshalala?
Kilichofuata usiniulize. Niliachana naye mwaka 2013 lakini mpaka leo ananipigia simu anataka niende aliko. duuuh!