Wizi wa mafuta kwenye vituo

sinafungu

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Posts
1,527
Reaction score
868
wadau wenye kufaham; kuna baadhi ya vituo hawakubali kabisa kuweka mafuta kwenye gallon za lt tano. na kuna baadhi ya vituo ukifika na usafiri wako tu(pump ni zaidi ya moja) utakuta wanakuelekeza pump maalumu, kwa mtazamo wangu kwa hayo mawili huwa nina shaka na kituo cha namna hiyo, labda tungejuzana kwa wale wenye uhakika na baadhi ya vituo salama.
 
Aise wezi kweli.Lakini siyo vituo kama vituo,wachakachuaji ni wale wanaopima.Wakubwa hawaelewi.Daresalaam ndo balaa.Wizi sana kwenye vituo vya mafuta
 
Nenda kituo cha puma pale sinza kijiweni ukifika utakuta pump zao hazijarudishwa ndani ili kuiresert manaining'iniza na usipoangalia vizuri utapimiwa mafuta ya elfu kumi kama ulitaka ya elfu ishirini nenda hadi sasa hivi wanafanya hicho kitu mabosi wao sidhani kama wanajua. Wanakera sanaa.
 
vituo vizuri vya kuweka mafuta ni 'engen,bigbon,vilivyobakia ni magumashi tu ,pia kama unaweka mafuta mengi tahadhari sana wanapokuongelesha,pia usikubali kuchaguliwa pump .
 
duuh...kituo cha ubungo pale mataa hakifai hata kidogo,ni maprofesianal wa kuchakachuA kituo salama ni total ya pale mliman cty na puma ya oceanroad
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…