Wizara ya Maji yasaini mkataba wa Tsh. Bilioni 15.6

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552


Wizara ya Maji imesaini mkataba wenye thamani ya Shilingi Bilioni 15.6 na Kampuni ya WAPCOS kutoka India ili kuanza kutekeleza mradi wa maji wa miji 29.

Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo, pamoja na Meneja Mkazi wa Kampuni ya WAPCOS Ltd, Bw. Chandrasekhar Kombathula wamesaini mkataba huo, wenye sehemu mbili, jijini Dodoma.

Prof. Mkumbo akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini amesema kazi hiyo inafanyika ukiwa ni mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya India kupitia Benki ya Exim ya India wenye thamani ya jumla ya Dola za Marekani milioni 500.
 
Tz Maji bado tatizo kubwa Sana ndio maana tukifanya tathimini ya ziara ya Mh.Dr.Magufuli utaona Kila Kijiji,kata,tarafa,Wilaya,Mikoa na Majiji watu wana changamoto ya Maji.
Tunaamini kupitia hii baadhi ya maeneo yatapunguziwa changamoto ya Maji,au kutatulia kabisa.
Naamini Prof.Katibu Mkuu,Waziri Prof.na bado wizara in engs.Wakutosha.

Pigeni kazi Wakuu!
 
Pesa ndogo,miji ni mingi labda kama kuna sehemu ni za kukarabari mitambo na nyumba zake
 
hivi masharti nafuu wapi na wapi?

hii mikataba ya ajabuajabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…