Kumeibuka biashara
jijini DSM ya kila kona ya jiji kuwashwa moto na kukaanga chips mitaani.
Wauza chips na mishikaki hawa hawafahamiki nani kawawapa kibali bila ya
kufahamu kama afya zao na mazingira ya biashara vinakidhi haja ya
kuwauzia wenzao vyakula. Biashara hii inawatia wananchi kwenye hatari ya
kuambukizwa magonjwa kama: typhoid, cholera, minyoo, na kuhara damu.
Pia, iko hatari ya mioto hii ya holela barabarani kuunguza waendao kwa
miguu kandokando mwa barabara pamoja na kuunguza nyumba zilizo karibu na
majiko hayo. Hivi wizara ya afya inasubiri mabaya yawapate wananchi
ndiyo ichukuwe hatua?