What will you niko njiapanda??

Aziz Ki Mayele

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2015
Posts
899
Reaction score
1,955
I Met a lady... kwa mara ya kwanza nikadhani she is just a woman to have fun with kwa hiyo haikua kitu serious, hakuna alietaka kujua situation ya mwenzake ya kimahusiano sababu we were just having fun

Baada ya muda mambo yakawa tofauti, nikaanza kumchukulia serious... Nikataka kufahamu kuhusu yeye na nikagundua alikua na mtu, yeye pia akabadilika she started being concerned tukakubaliana tuvunje mahusiano tuliokua nayo sababu within months tumekua na furaha and we really get along!!

Nadhani jamaa yake aligundua within time kwamba the lady was seing somebody else, kanitafuta contact zangu kazipata

The guy is begging nimuachie kwamba she have a plan with her na wanafuture pamoja, he is desperately begging na kunifanya nijisikie guilty... Nilipojaribu kumshirikisha demu she says she is staying with me!!

I have grown fund of her and I think we were building something so strong

Naombeni ushauri maana at the other side sms za jamaa zinanifanya nijisikie vibaya sana!
 
Na ww ndio wa kumshUri aachane na ww ili ajenge future na mshikaji, mimi demu alinibwaga kwa sababu ya hali ya uchumi matokeo yake demu nagonga kisela mpaka sasa, sijisikii vibaya coz she was my dream woman, jamaa ndio aliningilia kwenye anga zangu
 
Hii nimekupa athari ya ku "huck" madem za watu coz mapenzi ni ujinga fulani ambao ni ngumu kuuelezea, so linapokuja suala la kuoa ni jambo jingine, Ila kama just for fun, ila jipende ndugu yangu, usiendeshwe na hisia, zitakuua
 
uchumi wako upoje kwa sasa?
 
Hela ya kubadilisha mboga, kujenga na kuendesha subaru inatosha kwangu, sipendi mbwembwe
 
Let heart decided ur fates !!.

Angalia moyo wako ,,km unaumia kumchukukia jamaa Basi muachie
 
Jua kuna kitu kinaitwa KARMA my friend lazima.Itakurudia.. Sio vizur kufanya hvyo ni vyema kuwa na mahusiano yatakayo kupa Amani
 
Hivi hawa mademu ambao mnafikia hatua ya kunegotiate mtu akuachie mara demu achague, hivi huwa kuna mapenzi ya kweli hapo?!
 
TAFUTA WA KWAKO!! SIKITIKO LA HUYO JAMAA ONE DAY LITAKUA LAKO!!
 
Sipati picha jamaa atakua na hali gani mpaka kufikia kukutafuta
 
Yaani manaamke yalivyojazana hapa nchini, bado kuna wapuuzi wanalia waachiwe wanawake ambao tayari sio waaminifu kwao?

Ujinga Mzigo.
 
"How you get them, is how you lose them."

Ngoja nikuambie kitu, hakuna mahusiano matamu kama ya ngono. Tena iwe wote mnaibia. My friend unaweza kuhisi huyo ndo soulmate. Sasa wacha muwe wawili na hujui chochote kuhusu mwenza wako maana mlikuwa mnakutana kwa ngono tu. Hapo ndipo utagundua uliyekuwa naye alikuwa bora maradufu.

Sikukatazi kuendelea naye na wala neno langu si sheria, ila 99% ya mahusiano kama yenu huwa hayafiki mbali.

Lakini ngoja nikushauri pia kama hiyo 1% iliyobaki.

Fanya hivi;
Achaneni kwa muda. Muache akaachane na jamaa yake kwa sababu hataki kuwa naye (not kwa sababu kakutana na wewe). Na wewe pia ikupe muda wa kujitafakari maana nawe umeachana na mwenza wako kisa mwanamke huyu. Wakati anasafisha nyumba yake, kaa chini na wewe usafishe yako ukitafakari ni nini ulichojifunza huko ulikokuwa. Ni nini tofauti umekiona kwa huyu. NB: Hamuwezi mkahamia kwenye nyumba ambayo wapangaji waliopita bado hawajatoka, vivyo hivyo na moyo.
Kisha baada ya miezi michache (tufanye siku 90) mtafute muongee. Mkutane sehemu ya wazi na muongee kama mnaanza upya. Simaanishi muanze kutongozana ila muongee mnajisikiaje baada ya kukaa siku hizi 90. Kama hisia zenu kwa kila mmoja bado zitakuwa na nguvu basi anzisheni uhusiano wa ukweli sio unaoegemea ukuta wa ngono pekee. Kisha ningekushauri muanze tu mchakato wa ndoa maana naona upo tayari.

Nikutakie kila la kheri katika ukuaji..hii phase yako ni ngumu sana! Ila kama utaweza ushauri wangu ni mmoja tu, acha zinaa hasa kwenye mahusiano mapya/machanga. Utagundua mengi sana kuhusu mwenzako - mapema - kuliko mkianza mahusiano sekunde hiyohiyo mkaingilia mlango wa ngono.

Wasalaam.
 
ushauri gani unataka, acha ujinga, achana na mpenzi wa mtu, heshimu mahusiano yao.... kwani wanawake wameisha, na wewe siutafute mwingine? mpaka ujiwekeweke hapohapo kwa mpenzi wa mtu!!!!

Narudia tena, Acha ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…