Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,698
- 1,781
Kikawaida mwanaume unatakiwa uwe wa kwanza kwenda kupima kabla wife hajaenda, ukikuta ndivyo sivyo unafanya kumwandaa mapema.
Ila kiukweli ukimwi unatisha, inabidi upate counseling ya kueleweka si mchezo.
All in all, Ukimwi wa siku hizi hauui kama zamani, ukijikubali ziko njia za kueleweka za kuishi nao.
Mtego wa Noti hicho kijiji nimekivulia kofia, nimeshtukia nimecheka kwa sauti ofisini mpaka watu wamenishangaa aisee.Umeongea vizuri sana Kanigini, tatizo wanaume wengi tunaogopa kwenda kupima na badala yake tunawatanguliza wake zetu ndio wakapime ili watuletee majibu. Yaani akina mama huwa nawavulia kofia maana akiwa mjamzito tu apende asipende lazima apimwe HIV. Nakumbuka Morogoro sehemu moja vijijini huko kuna kijiji wana sera yao kuwa mama mjamzito lazima aende na mme wake kupima. Sasa kuna jamaa mmoja mke wake alikuwa mjamzito, mke alienda kupima ila jamaa aligoma kwenda kupima mpaka akawa anajificha maporini. Baada ya kuona vile ilibidi mtendaji wa kijiji atume mgambo wakamkamate na kumpeleka kituo cha afya kupima akiwa na mkewe! lengo likiwa ni kulinda mtoto aliyeko tumboni. Hii ni balaa kwa kweli! sasa sikuuliza kama alifanyiwa Counselling baada ya kupelekwa na mgambo kituo cha afya!
Mtego wa Noti hicho kijiji nimekivulia kofia, nimeshtukia nimecheka kwa sauti ofisini mpaka watu wamenishangaa aisee.
Hii inatakiwa iaplai kote ili wanaume waanze kuwa responsible kwenye michepuko.
Mode for christ sake ifunge hii mada
Mode for christ sake ifunge hii mada
Hata mi namshangaa huyu mdau anayetaka ifungwe!...Hii ni thread ya kuwafunza watu!Maada ya 2011 Septemba! Umeiona leo unalalamika ifungwe!
Hupati cha kujifunza humu kwenye hii maada?
Inaonekana inawastua wengi! Wengine hawapendi kwenda kliniki!Unaogopa nini?
Duuh! kweli huo ni
ukweli mchungu! hapo sasa magonjwa ya zina kama kaswende yameandikwa
wapi?
Niliwahi kupata kaelimu kidogo kuhusu hii makitu. Wenyewe wanasema hiyo ya kutumia PMTC 1,2,3....... ni namna ya kuwasiliana wao wakunga juu ya hali ya mama mjamzito na maambukizi ya VVU.
PMTC ikifuatiwa na namba shufwa (even) ina maana yake na ikifuatiwa na witiri (Odd) ina maana yake.
walikubaliana kutumia haya mafumbo kama njia mojawapo ya kupunguza unyanyapaa baada ya + na - kuwa common.
Hii mada kiboko aisee, kuna watu watajipiga kitanzi humu
Sawa kabisa Mfa maji, huwezi kundikiwa tu halafu ukambiwa nenda, ni lazima upewe ushauri hata kabla ya kuambiwa. Cha msingi tu watu tupende kwend clinic na wake zetu ili kama ni kupima na kupta ushauri tupate wote na siyo kuwatanguliza wenzetu kama chambo.Ninavyojua mimi hauandikiwi tu kwenye card ya clinic, unapewa kwanza majibu na ushauri nasaha. Mpaka ikiandikwa hivyo muhusika kazima ujue. Afterall si jambo la kuhofia kama zamani ni kufuata ushauri tu
Hii mada kiboko aisee, kuna watu watajipiga kitanzi humu
sasa hapo umezungumza kihesabu zaidi, kati ya 2 na 1 ipi shufwa na ipi witiri? najua wengine hesabu zilipita kando...Hizo Witiri na Shufwa zinaweza kupewa maana ya + na - . for the time being shufwa = +.
sasa hapo umezungumza kihesabu zaidi, kati ya 2 na 1 ipi shufwa na ipi witiri? najua wengine hesabu zilipita kando...
...Ooooh...hapo sasa nimekuelewa mkuu!Shufwa ni namba yoyote inayogawanyika kwa 2 na Witiri ni kinyume chake!