Wezi wavamia wodini, wawaibia wagonjwa simu, mikoba

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,853
Reaction score
14,082

Moshi. Watu wawili wanaodaiwa kuwa vibaka, wamevamia kwenye wodi namba moja katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT mjini Moshi na kuiba vitu mbalimbali ikiwemo simu za mkononi na fedha taslimu.

Watu hao ambao inadaiwa walikuwa wawili, waliingia katika hospitali hiyo leo alfajiri Machi 25, 2019 majira ya saa 10:00 na kuiba vitu hivyo ambavyo ni mali za wagonjwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamisi Issah amethibitisha kutokea tukio hilo na kudai watu hao wawili ni vibaka.

Akizungumza shuhuda wa tukio hilo, Rebeca Msigiti ambaye alikuwa msaidizi wa mgonjwa katika wodi hiyo, amesema watu hao ambao ni wanaume, waliingia wawili ambapo mmoja alibaki mlangoni na mwingine akaingia ndani na kuchukua simu za wagonjwa na mikoba yao.

Amesema watu hao walipoingia wodini wao walidhani ni madaktari wameingia, kumsaidia mgonjwa ambaye alikuwa amezidiwa.

“Watu hao waliingia wawili na tulidhani ni madaktari, ghafla tukaona wametoa simu zilizokuwa kwenye chaji na zilizokuwa kitandani na kuchukua pochi na kuondoka,” amesema Msigiti.

Source:- Wezi wavamia wodini, wawaibia wagonjwa simu, mikoba
 
Aisee sasa nimeamini kweli vyuma vimekaza watu wanapiga dili mpaka hospitali

CC Zero IQ
 
Wakawaona wanachukua simu na pochi wakawaangalia?? Aisee
 
Reactions: BAK
Ila nasi wagonjwa tupunguze manjonjo ..kutaka ku snapchat adi wakati wa kuchomwa sindano dunia ijue unaumwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…