Wewe dada, hizo mbinu Kimagharibi zitakugharimu...

mitale na midimu

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2015
Posts
10,419
Reaction score
17,765
kwa Muda kadhaa kwenye mtaa mmoja kwenye viunga vya jiji la dar es Salaam, ameibuka mwanadada mrembo na kuweka kituo kandokando ya barabara kwa shughuli inayosadikiwa kuwa anajiuza.

ikifika asubuhi anakuwa upande ambapo watu wenye vyombo vya usafiri wanaelekea kazini na kusimamisha kila gari (private). Huku akiwa amebeba mkoba wake uliojaa vipodoresho ambao baadae jua likizidi ataonekana amekaa chini ya mti anajikwatu.

Ikifika jioni anahamia upande wa pili, kusimamisha magari watu wanapokuwa wanarudi kutoka makazini.
Tabia hii, mara ya kwanza nimeiona kwenye movie za kimagharibi.

Kwa sababu humu jf nimejifunza ufukunyungu na ufuatiliaji wa mambo yasiyorasmi mara moja moja, ilibidi nifuatilie kwa mdau mmoja mwenyeji.

Akaniambia Lile ni Pepo, pepo la ngono haiwezekani mwanamke akawa hana aibu kiasi kile. Katika kumdodosa akasema wanamfahamu na wamama wa mtaani wameshakaa kikao kuona jinsi ya kumvizia na kumtandika bakora ahame kabisa hapo mahala maana ananajisi maeneo yao pia anawaweka waume zao katika hatari ya kuchepushwa.

ni muda mrefu imepita kama wiki mbili simuoni, najiuliza alikutana na kichapo akakimbia, au biashara haikunoga, au amehamisha kijiwe. Ila kama bado uko na huo mradi mkuudada nakuomba uhamishe offisi maana umeleta kero kubwa kwenye barabara yetu pendwa.
 
Wakat mwingine ujinga nikwa mwanamme , ww umeshaona huyu anajiuza kwann usivae mawani??. Kuna ulazima wakupagawisha naye , km nilift mpe, mambo mwngine kataaa, nakm unawazia nimwizi Usimpe lift kabisa...Simple mbona.

Alafu wacheza pono niwanawake ila wanakua wameshamua kua iyo ndo kazi yao ivyo hawana aibu .

Sasa uyo dada yeye hana kazi nyingine nakeshaamua kutumia iyo mitego kuishi.

Niujinga wa hao wake zawatu kumvizia mdada huyo nakumpa kipigo ili hali wanapaswa kuwaishi wanaume wao such that wasiingie ktk mitego huo ,, Nasio huo tuuu , kwan hamchepuki ???? Mbn mnachepuka sanaaaaaa tuuu??

Kwaiyo kutoka kwangu nasema , Hata hao wake zawatu nimajinga tuuu., kwan yeye atajua huyu kaoa uyu hapana ??

Yeye yupo kazini kwake basi , tena bora uyo wa mchana mchana ili umuone umjue .

Sisetei ukahaba , ila ww mwanamme umeoa au unamchumba wako , hata kama hutomwopoa uyo dada Changu ,lkn Unachepuka,unamademu kumi kumi ,HUO NAO NI UJINGA.
 

Una tabia za kike
 
Akijiuza yeye ....taifa linapata anguko LA uchumi... Ungefafanua vizuri....kama sio mfadhaiko wako wa kingono ...lengo lako nn ???
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…