hebu chukulia kuwa umeoa halafu mkeo mkahitilafiana, je suluhisho ni kumtafuta mume bora umkabidhi mkeo mpaka atakapotengemaa kitabia? fikiri kabla ndugu yangu.... (kwa ufupi hautapata kura yangu ng'o)Imedhihirika kwamba Viongozi waTanzania nchi imewashinda...Mnaonaje tukaingia mkataba na nchi moja ya Magharibi iliofanikiwa kiuchumi kuendesha nchi yetu kwa miaka 100 ili kuboresha Maisha ya Mtanzania..Miaka 100 ya kujenga mabarabara,shule,hospitali na mengine muhimu...na wao wawe na full control ya kila kitu..vipi wadau mnaonaje hio?
well said nakuunga mkono mkuuSikubali: Kwanini usiende huko ili mimi nibaki na TZ yangu? Kwanini usisema tuwafukuze wote? Ishi yaani wanibinafisishe? Wewe vipi?
unaichukulia serius ile kauli ya kwamba mali zilizomo humu nchini ni urithi wa taifa? na warithi ndo sisi? well ni kwamba ukishauza nyumba yako uliyojenga na kuishi bila maandalizi ya uendako basi hiyo ndo akili tata, au mwenzetu umejiandaa kutimkia bara lipi? au utaenda kuishi kenya?Mimi naona bora tuiuze tu kila mtu apate chake na sio kila siku RA, RA, EL
Wanaingia mikataba ya hovyo ya kufua umeme na kuchimba madini ambayo baada ya kuisaini tunakuwa hatuna tena uwezo wa kuifuta au kuisitisha. Je, wakiingia mkataba wa kuibinafsisha nchi una uhakika gani kuwa baada ya miaka 100, hata kama hayo maendeleo yatakuwa yamepatikana, tutakuwa na uwezo wa kuirudisha nchi mikononi mwetu? Upunguani unaotufanya tushindwe kuendesha nchi ndiyo huo huo utakaotufanya tushindwe hata kuidai tena nchi yetu. Wewe kama unataka kurudi nyuma ya mwaka 1961 rudi mwenyewe sisi tutapambana na mafisadi wetu. Swali? hivi wewe binafsi umefanya nini kukabiliana na changamoto za matatizo?
Imedhihirika kwamba Viongozi waTanzania nchi imewashinda...Mnaonaje tukaingia mkataba na nchi moja ya Magharibi iliofanikiwa kiuchumi kuendesha nchi yetu kwa miaka 100 ili kuboresha Maisha ya Mtanzania..Miaka 100 ya kujenga mabarabara,shule,hospitali na mengine muhimu...na wao wawe na full control ya kila kitu..vipi wadau mnaonaje hio?