Waziri Makame Mbarawa, wananchi wa Wami Dakawa umetuangusha hatuna imani na wewe

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,856
20,708
Professor Mbarawa pole na majumu ambayo nadhani ni magumu hasa ukizingatia utendaji wa Rais wetu wa awamu ya tano uliotukuka.Anyway tuachane na hilo twende kwenye point.

Si muda mrefu sana ulitembelea mradi wetu wa maji wa Wami Dakawa,au kwa sababu ya taarifa ambazo ulikuwa umeshazipata kuhusu utendaji mbovu wa mradi huo au katika utendaji wako wa kawaida tu.Tunashukuru kwa kufika na kuthibisha kwamba kweli kuna matatizo.Matatizo ya mradi huu ni ya siku nyingi.Kiukweli tangu umeanzishwa haujawahi kuwa na ufanisi,pamoja na kwamba viongozi wa Kijiji,Kata,Tarafa,Mbunge na Halimashauri wapo.

Katika hatua za awali kabisa watu walichota hela,wengine wakahamishwa bila kuchukuliwa hatua yeyote na wengine katika hali ya kushangaza wakaachwa waendelee na kazi.Tatizo la kujichotea fedha za mradi huu bado lipo,na wewe ulipokuja naamini ulilibaini,ukaahidi kwamba utaleta watu wako wafanye uchunguzi zaidi wa kina,lakini cha ajabu hakuna uchunguzi wa kina uliofanywa,viongozi wale wale wapo,it is business as usual.Hatukuelewi ndugu Waziri.

Waziri naomba nikupe taarifa kwamba tatizo la mradi huu linasabishwa na viongozi Wilayani,kwa hiyo kama una nia ya kweli ya kuongeza ufanisi wa mradi huu, uchunguzi uanzie huko.Viongozi hawa badala ya kuuwezesha mradi kwa kuuongezea mtaji hasa wa umeme,wao wanachota.

Waziri si vibaya kuku kumbusha matatizo mengine ya mradi huu,ingawa naamini unayajua.Mradi hautoi maji kwa wananchi masaa yote,on average unatoa maji kwa masaa mawili tu na wakati mwingine hakuna kabisa!Pia mawasiliano kati ya watumia maji na mradi ni kidogo sana na ufuatiliaji wa matatizo yanapotokea ni hafifu sana,kitu ambacho kina athiri upatikanaji wa maji katika hizo saa mbili ambapo maji yanapatikana.

Mwisho tunaomba unapokuja uwe na audience na wananchi,ukifanya hivyo itakuwia rahisi wewe kama Waziri kupata first hand matatizo yanayowakabili wananchi katika miradi yao.

Naomba baada ya kusema hayo nikutakie kila la heri katika utendaji wako.
 
Back
Top Bottom