Daktari bingwa wa afya ya kinywa na meno kwa watoto wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Conrad Mselle ameishauri jamii kutokumwacha mtoto alale na chuchu ya mama mdomoni hasa wakati wa usiku kwa kuwa bakteria wanaoishi mdomoni hutumia sukari kuzalisha tindikali inayosababisha meno kuvunjika.
“Niwashauri wazazi kusafisha vinywa vya watoto wao mara baada ya kuwapa dawa za maji (syrup) kwa kuwa kutokufanya hivyo bakteria huitumia kuzalisha tindikali na kuharibu meno,” alisema Dk. Mselle.
“Niwashauri wazazi kusafisha vinywa vya watoto wao mara baada ya kuwapa dawa za maji (syrup) kwa kuwa kutokufanya hivyo bakteria huitumia kuzalisha tindikali na kuharibu meno,” alisema Dk. Mselle.