Watuhumiwa wanne wahukumiwa kifungo cha miaka 360 jela kila mmoja

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Mara leo imewahukumu Watuhumiwa wanne wa ujambazi wa kutumia silaha kutumikia kifungo hicho jela

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi, Staneley Mwakihaba baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na walalamikaji 12

Mwendesha mashitaka wa Jamhuri, Yese Temba aliiambia Mahakama kuwa Watuhumiwa hao wakiwa na bunduki aina za SMG, Panga na Shoka waliwavamia walalamikaji

Waliwatishia kuwaua na kuwapiga kwa kutumia silaha kisha kuwapora fedha na simu huku risasi moja ikimpiga Janipher Howard na kusababishia ulemavu baada ya kukatwa mguu

Katika tukio hilo lilotokea Desemba 02, 2016 katika kijiji cha Magunga wilayani Butiama mkoani Mara, Daniel Yuda alijeruhiwa kwa risasi katika mguu wake wa kulia

Chanzo: ITV
 
Hivi miaka 360 na kifungo cha maisha wana tofautiana??au ukifungwa miaka 360 unaweza maliza ukamwacha wa kifungo cha maisha akiendelea na adhabu
 
 
Kwahiyo wanazungusha nyuzi 360, yaani 360 degrees hadi duara likamilike? Aagh, clouds 360 kabisa?!
 
Miaka 360 gawia watuhumiwa wanne ndicho kifungo cha kila mmoja sio kama mlivyoeleza hapo juu wakuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…