heri waislam wao salam yao ni asalamaleyko kwishne hiyo.Mimi mgeni huku dsm, ukiachana na tabia ya wakazi wa huku kichukulia chips kavu kama mlo wa siku, bonanza kuchezwa mpaka na mabinti, madela kwa wingi!!
Kuna hii tabia ya kutokuitikia salamu. Inanikera, unakutana na mmama umri umeenda, unamwamkia, anakwambia kashike ya kwako, kamsalimie mama ako, unaamua kukaa kimya.
Juzi kuna mmama kanikuta barazani home, nikamwangalia tu, akawa ananangalia sana, nikajistukia nikamwambia, zas'aiz, akanambia kuwa na adabu!!
Mara watake salamu, mara hawataki!! Hadi mtu unashindwa ufanye nini, kupita kwa watu unaona balaa!!
Wenyeji wa huku tupeni mwongozo.....