'Watoto wa wakubwa' wajazwa Idara ya Afya; Washika nafasi zote za Jiji, Ilala, Temeke, K’ndoni

Kuhusu Mtoto wa Kawawa ameajiriwa Kama Daktari wa Jiji toka jiji ni Manispaa na amewahi kuwa Daktari wa wilaya ya Kinondoni tangu miaka ya tisini nafikiri kwa hapo alipo sasa anastahili kwani ameanza chini na anazaidi ya miaka Ishirini ya service Labda awe ni mwengine.
 
Waenga walisema mwenye nacho hatazidishiwa


Na ng'ombe wa maskini hazai akizaa basi dume, wote mnaolalamika hata kama ni wewe ungekua mtoto wa hao mnao waita vigogo kama sifa unayo utakataa hiyo nafasi kisa mzee wako ni KIGOGO
 
Watanzania bado tuna safari ndefu, uelewa bado ni mdogo sana, yaani mtu ameeleza kwa ufasaha juu ya watoto wa vigogo kupewa nafasi za upendeleo mijini, halafu vilaza wengine wasioelewa wanakurupuka kujibu na kutetea uovu. Rudini shule kwanza sio mnan'gan'gania tu kuandika pumba kwenye jamii forum
 

Wewe elimu yako mbona nayo ni ndogo,au unataka niseme?tatizo lenu ninyi Bwana mnajifanya mnajua kuwafuatilia sana wenzenu kuhusu maisha yao wakati hata ninyi maisha yenu ni machafu,halafu we kaka jiangalie utapewa za uso kumbuka tunakufahamu vizuri.

Lakini la pili,hivi kwa akili yako hiyo ndogo uliyoa nayo ulikuwa unataka baada ya hao watoto wa vigogo kusoma wakafanye kazi wapi???!!!,au ulikuwa unataka ukae nao n kuwanyanyasa kama ambavyo unawanyanyasa wale wenzako???
 

LOL... Unanifahamuje VIZURI USO WANGU? Wangapi Wamepewa za USO wakiwa Wachangiaji wa JAMII FORUMS?
HII INAONYESHA imekugonga NDANI ya KIWILIWILI chako kisicho na ROHO ila USO usiofahamika!
 
Mhhhh kwa hiyo interview zinavyoitishwa ni kutakatisha majina haya? Nakumbuka miaka ya 2000 BOT bodi iliweka pingamizi kwa watoto hawa wa vigongo walioajiriwa bila kufuata taratibu za weledi mana wengi wao hata vyeti vyao ni hitilafu na ukimwambia aandike report umeua kabisa!! Rubbish!!! Kiflichofuata ni Governor Bilal kuitisha interview ili kuwatakatisha!!! Yaani Bilal aliua kabisa ule utaratibu wa kuajiri kwa SIFA BOT na matokeo yake Seniors wanapata tabu sana kufanya kazi na hawa watoto wa vigogo!!! Ni wachache kati yao wana angalao minimum qualifications!!
 


FINALLY NIMEIPATA CISCO Trans.Matrix Nimepata IP ADDRESS yako; Sasa JIBU MASWALI kama KIONGOZI SIO USHABIKI... I do constructive criticism OF YOU
 
Ah mbona watu wanasema waislamu wanayimwa nafasi,mbona hiyo list wapo waislamu,nimesema hivyo kuwa jamani mambo ya dini hayabagui katika ajira muhimu uwe na sifa baaasi,ndugu zangununi tujitahidi kwa kula hali tuwasomeshe watoto wetu,waacha tuvae hata suruari za viraka lakini hakikisha unasomesha wanao,huo ndio utakuwa ukombozi kwa watoto wa kimasikini kulalama kila siku,maandamano hakutatufanya watoto wetu wapate ajira nzuri,huo ndio ukweli na asiyeukubali ameze wembe!
 

jamani nauliza tuu..hivi huyu mtoto wa malima ana misimamo ya babake?Babake ai alishashaungwa mkono ni vijana mamia waliokuwa tayari kuanzisha jihad ya kupindua nchi..Asijemchoma mtu sindano ya sumu ili asiwe mpinzani wa ndungu yake akikgombea Upresidaa.Si swali tuu si lazima kujibiwa.
 
nanyie msomeshe wa kwenu afu muingie kwenye system mfanye mambo.:shut-mouth::majani7:
 
Mbona JIBU ni rahisi sana;
Ili kupunguza urasimu wa kutoa recommendation, advise na referrals za viongozi (Ambao ni baba, mama zao na ndugu zao) kwenda kutibiwa nje ya nchi
 
Kinachoulizwa hapa ni kwa nini wao ni mijini tu na hawaendi huko mikoani na vjijini ili kutoa huduma kwa watanzania wenzao? na hao wenye elimu kama wao waliopo mikoani na vijijini kuja kutoa huduma huku mijini?
 

Andika kama mtu unaefualitia kwa ukaribu mwenendo wa utoaji wa elimu unavyokwenda katia nchi hii, hao unaosema wamesoma ni watoto wa vigogo na mikopo yao University ni 100% wa masikini hata mkopo apati na wengi wanashindwa. kuna shule za kata walimu 2 au 1 shule nzima na ndiyo shule za watoto wa masikini kwa hali hiyo usitarajie miujiza kwa mtoto wa masikini kupata elimu bora, kwani elimu ya nchi hii ni KANDAMIZI kama huduma zingine.
 
nikikumbuka hata SENSA NILIKOSA najionea huruma na kuichukia nch yangu
 
soma na wewe usilete wivu wa kijinga hapa wenzio wamesoma ulitaka wafanye nini??? jaji mkuu wa znz
aliwahi kusema watu wanaomsema kumpendelea mwanawe kuwa jaji wanamwonea kijicho cauz wao hawakusomesha wakwao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…