Watazamaje siasa za nchi yako? Unafikiri sawasawa?

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,366
11,157
Kama inavyojulikana mwanasiasa ni "perception"(jinsi jamii inavyokuona) kwa mfano kama watu wanakuona ni fisadi au mwizi hata kimakosa hitimisho ni kuwa hufai kuwa kiongozi, na hiyo ni hukumu tosha haiitaji kwenda mahakamani ili kuthibitisha usafi wako - kama upo kwenye uongozi achia ngazi.

Vivo hivyo kwa chama cha siasa kama wananchi wanakiona kwa mtazamo wao kina tabia ya kueneza chuki na migawanyiko au kulea ufisadi hukumu yake ni -hakifai kuwaongoza.

Kama pia wananchi kwa mtazamo wao wanaona siasa katika nchi zimekaa tenge na zina sura zote za uchafu, hukumu yao ni hazifai.

Pia kama wananchi kwa mtazamo wao wanaona kwamba wanaitizama siasa kifisadifisadi na kwamba na wao si safi nani awahukumu na hukumu yao ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…