Hii ilikuwa ni hotuba ya Baba wa taifa Mwl. J.K.Nyerere 1995 ktk mkutano wa CCM kumpitisha ngombea urais wa TANZANIA.
"Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Yapo mambo watanzania wanayataka uongozi huu uyafanye mengi tu. leo nitayataja matatu no manne.
1. WATANZANIA WAMECHOKA NA RUSHWA..
Wajumbe wa zamani watakumbuka nimelipigia kelele, kiasi Waziri Mkuu wa wakati huo alikuja kutoa hati yake ya kujiuzulu. Wasaidieni wananchi
2.NCHI HII NI NCHI YA WATU MASIKINI
Nchi hii ni ya wakulima na wafanyakazi wetu masikini, nchi hii haijawa ya matajiri
3.UDINI
Tulikuwa hatujali dini ya mtu, anaijua yeye mwenyewe dini yake basi. Hatukumpima mtu kutokana na dini yake ndio tumchague
4.UKABILA
Watanzania wanaulizana makabila, wanafikiri ni maana..mnataka kutambika?
Hii ndio Hotuba iliyomuondoa Ndg. Edward Lowassa katika nafasi ambayo angeshinda mwaka 1995.
Je, Mabadiliko tunayoyataka leo ni ukweli ama ulaghai?
CCM waliheshimu wosia huu kumpata MH. DR. JOHN POMBE MAGUFULI?
CHADEMA waliheshimu wosia huu kumpata MH. EDWARD LOWASA?
Wanaopiga kelele za mabadiliko wao wenyewe wanatakiwa kubadilishwa maana hawaelew wanachokihubir, :
1.Rushwa
Siku za nyuma nilikuwaga mfuasi mwaminifu wa Chadema, kilichonivutia zaidi ni yale mapambano yao dhidi ya rushwa na ufisadi,walipobadilika na kuanza kupokea wala rushwa na mafisadi nguli kama Lowasa nikaona hawakuwa na msimamo kwa yale waliyokuwa wanayasimamia.
2.Lowasa ana Mali nyingi ambazo kazipata kwa njia haramu, kuna taarifa kwamba waarabu wamemkopesha Fedha ili akishinda urais awalipe baadae, watanzania Hatuna Haja na huyu mtu maana atakuja kuuza nchi kwa waarabu wake
3.Lowasa anautumia udini kuusaka urais pasipo kujua kwamba nchi haina dini bali wananchi wake, tumemsikia akimwaga pesa kwenye nyumba za ibada ili apigiwe kura, alienda mbali zaid pale alipowataka waumini wa Lutheran wamchague kuwa Rais kwa kuwa yy ni Lutheran, mtu anayetumia dini kutugawa watanzania ni wa kuogopa kama ukoma,
4.Lowasa tumemsikia akisema toka uhuru hakuna Rais aliyewahi toka kaskazini hivyo watu wamchague yeye kwa kuwa anatokea huko, anajisahau kwamba Rais ni mtumishi wa wananchi wote bila kujali dini, rangi, kabila nk,..
Kwa kuzingatia maelezo haya ndugu Lowasa amekosa sifa za kutumia wananchi wa taifa hili, sio muadilifu, fisadi, mdini pia anaendekeza ukabila.