Watanzania, Tusiogope changamoto!!

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
36,507
Reaction score
45,129
Wakuu,

Hii hoja si ngeni, imeongelewa sana hapa nchini wageni wanakuja kupora fursa zetu. ukweli ni kwamba Dunia ya sasa watu ni dynamics - watu wanaingiliana katika masuala mengi sana, kwa hiyo watanzania tuanze kuwa na moyo wa kujiamini na tusiogope changamoto hizi zinazojitokeza.

Jana usiku katika kipindi cha Malumambano ya hoja ITV nimeona watu tena wanaoheshimika kisoka walilialia kwamba kuruhusu timu kusajili wachezaji 10 ni kuua soka la ndani, hasa hasa timu yetu ya taifa huku wakitoa hoja dhaifu kwamba wachezaji wa kigeni ndiyo watacheza dk nyingi uwanjani kuliko wa kwetu hence kuua ama kulimaliza kabisa soka letu - sasa jiulize hivi tuna soka llipi ambalo akina Asante Kwasi na wenzake watalimaiza?

Kuna suala pia la kufungua milango EAC, watu wengi tumekuwa na wasiwasi kwamba wakenya, waganda ni aggressive sana kwamba watakuja kuchukua ajira zetu na pia wao wana uzoefu mkubwa kwenye mambo ya Kilmo, Ufugaji, Viwanda nk Kuwaruhusu hawa tutajikuta ardhi yetu yote wanamiliki wao na sisi tunakuwa wafanyakazi kwenye mashamba yao.

Sasa ndugu zangu huu woga mpaka lini? mimi nawashauri kwamba binadamu bila kupitia changamoto hawezi kupata maendeleo, kama umefanya kitu kwa miaka 40 na unataka kuendelea kufanya namna ile ile basi wewe una matatizo makubwa.

Tufungue milango kwenye sekta zote na tuwe tayari kwa mashindano, mchina njoo, mkoria njoo, mkenya njoo ili tushindane hapa hapa, Dunia ya leo huwezi kujifungia ndani uchumi wa leo utakutoa kwenye reli tuache mawazo ya zile zama za miaka ya 70 kweusi wakati wa TAA hizo zimeshapita na hazitakaa zirudi tena.

Nawakilisha - Watanzania tupambane, wao wanaweza sisi tushindwe tuna nini? tuache kulia lia na nawapongeza TFF kuja na wazo hili kwa ujasiri mkubwa - Hongereni sana.
 
Nimependa sana hapo uliposema kama utafanya jambo kwa miaka 40 afu unataka kuendelea vile vile hamna mabadiliko utakuwa na matatizo notice na pia kwenye maisha usipopitia changamoto hupati maendeleo pia ukasema watakuja wakenya na waganda kuchukua aridhi yetu kutokana na wao wako vizuri kwenye masuala ya kilimo,ufugaji viwanda na n.k sasa kinachonipa utata yaani ambapo sijaelewa umesema wachina kuja wakenya kuja sasa wakija na wao wako vizuri kama ulivyosema huoni suala la sisi kufanya kazi kwenye mashamba yao iko pale pale tena tukiwa nyumbani ...aridhi mama nielewesha hapo cjakupata
 
a
Hapo ndipo wasiwasi wa wengi wetu ulipo, kama ukisharuhusu hayo utatunga kanuni zitakazofuatwa, kwa mfano mgeni hawezi kumilikishwa ardhi wa miaka 20 lets say, sasa atafanya kazi baada ya miaka hiyo kuisha shamba linabakia kuwa lako, miundombinu na ujuzi juu kakuachia - Je utakuwa umepoteza nini hapo?

Hata kwa wale wachezaji wageni, lets say Simba ina wachezaji 10, unaweza kuweka kanuni kwenye mechi za ligi yetu ni wachezaji wa kigeni 5 tu wanaruhusiwa kucheza na mechi za kimataifa ruksa kuwatumia hata wote 10. Vilevile itaongeza ushindani kwa wachezaji wetu k- huwezi kupata mafanikio changamoto kitu hicho hakipo duniani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…