Watanzania nchini ugiriki

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,113
Reaction score
34,953
SUPER STAR WA TAARABU WA TANZANIA BIBIE KHADIJAKPOA ALIPOTEMBELEA NCHINI UGIRIKI.



Kumbe bibie Khadija kpoa ma la nguvu mashallah namzimia kweli...............
 
Timu ya Taifa ya Tanzania nchini Ugiriki Taifa Star.



Huyu ndie Kocha wa hiyo timu kana unaweza kumjuwa alikuwa Mchezaji wa timu ya coastal Union ya mjini Tanga simtaji kwa jina. jina lake linaanzia kwa herufi ya kwanza ni K na ya mwisho ni S.
 




MAREHEMU ASHA KALLENGA ALIYEFARIKI NCHINI GREECE AMEZIKWA LEO 18/06/2012 KWENYE MAKABURI YA KISUTU DAR.
TUNAWASHUKURU WALE WOTE WALIOSHIRIKI KUUFIKISHA MWILI NYUMBANI
MWENYEZI MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMIN.


MWILI WA MAREHEMU JAMHURI TUMEUSAFIRISHA LEO.

Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na jitihada zetu tumefanikiwa kumsafirisha marehemu HAROUN ABDALLAH OTHMAN (Maarufu kwa jina la JAMHURI) ili akazikwe nyumbani.Mwili wa Marehemu utawasili Dar Alhamisi 01/03 saa nane na nusu usiku kwa ndege ya Turkish airline (TK603)

Pamoja na hali ngumu inayoendelea kutukabili watanzania tunaoishi ugiriki ugumu huo


Jumuiya ya watanzania ugiriki inasikitika kutangaza kifo cha mwenzetu HAROUN ABDALLAH OTHMAN (Maarufu kwa jina la JAMHURI)kilichotokea hospitali ya Nikeas Piraeus J'mosi 18/2/2012. Marehemu kabla ya kuwasili ugiriki alikuwa ni mkaazi wa Kikwajuni Zanzibar. Hivi sasa tupo katika harakati za michango ya kutuwezesha kumsafirisha nyumbani.
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi Amin.
INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUUN

Kayu Ligopora
KATIBU MKUU
Jumuiya ya watanzania Ugiriki
 


KWA KUWA 12/01 WATU WENGI TUTAKUWA MAKAZINI JUMUIYA YETU IMEAMUA SHEREHE YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IFANYIKE SIKU YA JUMAMOSI: 14 JAN 2012 KWENYE OFISI YA JUMUIYA -LEMESOY 1 ATHENS - KUANZIA SAA:22.00 HADI ASUBUHI . KIINGILIO NI YURO 5 TU SHEREHE HIZO ZITASINDIKIZWA NA WASANII WETU MIKE JACKSON NA SANDRA .AIDHA KUTAKUWA NA SPEECH MAALUM ITAYOTOLEWA NA WAKUBWA WETU. TUNAWAOMBENI MHUDHURIE MAPEMA.

KHADIJA KOPA ATATINGISHA ATHENS IJUMAA 23/12

Jumuiya ya watanzania Ugiriki baada ya kuhakikisha imekamilisha hatua zote za kumwalika Malkia wa Mipasho (KHADIJA KOPA) inapenda kuwafahamisha wale woote waliokuwa na hamu ya kuja Athens kuhudhuria show maalum ya Malikia huyo WASISITE KUJA. Tunawaarifu kuwa hatua zote za viza zimekamilika na tiketi yake pia ipo OK. Atawasili Athens Alhamis jioni na Ijumaa 23/12 kuanzia saa nne usiku hadi alfajir atatumbuiza katika ukumbi wa AXUM uliopo mtaa wa DROSOPOULU 183 kwa kiingilio cha yuro 20 tu.
Tuna mipango ya kumpeleka nchi jirani akatumbuize kabla hajarejea nyumbani wiki ijayo.

(KAYU LIGOPORA)
KATIBU WA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI
 







TUTAKUKUMBUKA DAIMA, ASHA KALENGA UMETOA MCHANGO MKUBWA KATIKA KUIJENGA JUMUIYA YA WATANZANIA UGIRIKI, TUMESOMA MINGI KUTOKA KWAKO, TULIKUPENDA, TUTAENDELEA KUKUPENDA ILA MOLA KAKUPENDA ZAIDI, MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA PEPONI AMEEN.. WATANZANIA TUNATAKIWA KUKUTANA SAA 19:00 HAPO OFISINI LIMOSOU 1. KUPEYANA HABARI ZAIDI KUHUSU MAZISHI. AHSANTE.
 

HII NI MOJA YA KUMBUKUMBU ZAKE ALOTUACHIA DADA YETU ASHA KALENGA, Tutakukumbuka kwa mengi, sisi tulikupenda na tutaendelea kukupenda ila Mola alikupenda zaidi, Mungu akulaze mahali pema peponi Ameen...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…