Watanzania masikini tupimwe mkojo

LUTENI MUSSANTE

New Member
Joined
Nov 5, 2017
Posts
2
Reaction score
0
Salaam wajumbe!!


Nianze kwa kumshukuru muumba mbingu na nchi kwa hii pumzi maana ni wengi kwa macho yangu nimeona wakitamani hii pumzi ila mungu akawapenda zaidi.

Niende moja kwa moja kwa mada kama heading inavyosema 'Watanzania masikini tupimwe mkojo'.Taifa hili ni changa sana licha ya kupata uhuru miaka 56 iliyopita mchakato wa kulitoa taifa masikini kuwa taifa tajiri sio wa muda mfupi kama graduate wa chuo kikuu anavyoaamini kuwa baada ya kupata kazi ndani wa mwaka mmoja atakuwa billionaire(upeo finyu kabisa).

Jitiada zimefanywa na zinaendelea kufanya na viongozi wetu licha ya watu wachache wenye maslai binafsi kukejeli jitiada hizi.Nipende tuu kumpongeza raisi John Pombe Magufuli kwa hili japo wachache wenye masirai binafsi hawaona mchango wake.Niweke tuu wazi kuwa anachokifanya raisi kwa sas yawezekana ww usione impacts zake ila amini kuwa mtoto au mjukuu wako atakuja kuona.

Embu turudi katika vitabu vya historia,mfano tuangalie taifa kama Marekani limepata uhuru mwaka 1776 kutoka kwa Mwingereza jitihada nyingi zilifanywa na rais G Washington kama vile kuanzisha Isolation policy kwa kipindi kile wengi hawakunufaika nayo ila leo hii tunaona matunda yake.

Kuna kitabia kimezuka miaka ya hivi karibuni hapa Tanzania kuna watu wachache wanatumia changamoto za waliowengi kujijengea umaarufu na sie masikini tulivyokuwa wajinga basi kila jambo lisemwalo na hao wachache tumetokea kuwaamini.Hivi inakuaje mtu tena masikini unaacha kufanya shughuri za maendeleo unakazi ya kumfatilia Mange Kimambi ambaye yeye maslai yake na yako ni tofauti.
 
Hivi inakuaje mtu tena masikini unaacha kufanya shughuri za maendeleo unakazi ya kumfatilia Mange Kimambi ambaye yeye maslai yake na yako ni tofauti.

mmh hii sehemu ya mwisho ndo inanifanya kuwaza sana.
 
Hivi inakuaje mtu tena masikini unaacha kufanya shughuri za maendeleo unakazi ya kumfatilia Mange Kimambi ambaye yeye maslai yake na yako ni tofauti.

mmh hii sehemu ya mwisho ndo inanifanya kuwaza sana.
Kwanini kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…