..Woga ..nidhamu ya woga!! dawa yake ni ipi?
Wengi mtakubaliana nami kuwa kwa sasa sio humu JF peke yake hata maofisini, nyumbani, vyuoni n.k. tumekuwa na ushabiki mwingi wa kisiasa na kutambiana kuwa chama flani kimeshinda bila kuangalia kimeshindaje na kinatupeleka wapi, mengiyamesemwa ya kweli na si ya kweli kuhusu vyama mbali mbali...sasa hivi tunacheka na kurelax, ila wakati utakapowadia tutalia na kusaga meno...hii nidhamu ya uoga tuliyo nayo ndo inayotufanya tukandamizwe na mfumo wa siasa uliopo madarakani. Simaanishi tuingie msituni, ila tuelimishane na kuhakikisha kuwa huu mfumo dhalimu unaondoka....Mi nshaanza kuchukua hatua kivyangu, soon mtanisikia nitakapolipuka. Nimechoka kuishi ka mkimbizi kwenye nchi yangu.
Nikubaliane na wewe kwamba kwa kiasi kikubwa kinachochangia kuendelea kutawalia na wakoloni wazawa ndani ya nchi yetu ni WOGA WA KUTHUBUTU sijui ndo hicho unachokiita nidhamu ya woga? Ndugu zangu kama elimu kwa kweli vyombo husika vimejitahidi sana. Watanzania wa leo, wengi ukiwauliza sababu za uduni wa maisha yao watakuambia kwa asilimia kubwa zinasababishwa na mfumo wa utawala/uongozi wakiwa na maana uongozi bado haujajitoa ipasavyo kutumika kwa maslahi ya umma. Lakini, watajitoaje ili hali hawajui kwa nini twaishi kwa shubiri badala ya asali.Wengi mtakubaliana nami kuwa kwa sasa sio humu JF peke yake hata maofisini, nyumbani, vyuoni n.k. tumekuwa na ushabiki mwingi wa kisiasa na kutambiana kuwa chama flani kimeshinda bila kuangalia kimeshindaje na kinatupeleka wapi, mengiyamesemwa ya kweli na si ya kweli kuhusu vyama mbali mbali...sasa hivi tunacheka na kurelax, ila wakati utakapowadia tutalia na kusaga meno...hii nidhamu ya uoga tuliyo nayo ndo inayotufanya tukandamizwe na mfumo wa siasa uliopo madarakani. Simaanishi tuingie msituni, ila tuelimishane na kuhakikisha kuwa huu mfumo dhalimu unaondoka....Mi nshaanza kuchukua hatua kivyangu, soon mtanisikia nitakapolipuka. Nimechoka kuishi ka mkimbizi kwenye nchi yangu.
Lipuka mwenyewe, hatutaki shari Watanzania.
ndg yangu leornado, nakupongeza kwa topic yako yenye kuleta ujasiri. Ndg zangu wapenda maendeleo, wengi wameongea mengi kuhusu tanzania yetu kuhusu utawala ulioko madarakani, mengi yamesemwa na yanaonekana kwa macho.
Watu wengi wanateseka ktk nchi hii na hawana mwelekeo ktk maisha yao ya kila siku. Ili mwamini bw leornado anasema kweli tuliambiwa mtanzania atapata milo mitatu kwa siku inakuwaje mtanzania anaishi chini ya dollar 1 kwa siku, ndio maana kuna usemi huu wametupima viatu mwaka huu na baada ya miaka mi5 mtaulizwa mna vaa namba ngapi. Wanzania tujipange tuwe na ujasiri tujikomboe na maliza kwa kuuliza swali. Umekutana na mamba mtoni kukimbia ni vigumu je utajitoa sadaka kwa kujitupa mtoni au utapambana mpaka tone la mwisho la damu yako?
wewe ndio walewale mkisikia kulipuka mnafikiri mabomu. si ndiyoLipuka mwenyewe, hatutaki shari Watanzania.