Watanzania kenueni meno sasa na kubezana badala ya kuchukua hatua, TUTASAGA MENO!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watanzania kenueni meno sasa na kubezana badala ya kuchukua hatua, TUTASAGA MENO!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Leornado, Nov 23, 2010.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wengi mtakubaliana nami kuwa kwa sasa sio humu JF peke yake hata maofisini, nyumbani, vyuoni n.k. tumekuwa na ushabiki mwingi wa kisiasa na kutambiana kuwa chama flani kimeshinda bila kuangalia kimeshindaje na kinatupeleka wapi, mengiyamesemwa ya kweli na si ya kweli kuhusu vyama mbali mbali...sasa hivi tunacheka na kurelax, ila wakati utakapowadia tutalia na kusaga meno...hii nidhamu ya uoga tuliyo nayo ndo inayotufanya tukandamizwe na mfumo wa siasa uliopo madarakani. Simaanishi tuingie msituni, ila tuelimishane na kuhakikisha kuwa huu mfumo dhalimu unaondoka....Mi nshaanza kuchukua hatua kivyangu, soon mtanisikia nitakapolipuka. Nimechoka kuishi ka mkimbizi kwenye nchi yangu.
   
 2. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  ..Woga ..nidhamu ya woga!! dawa yake ni ipi?
   
 3. L

  Leornado JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tumekuwa waoga, tunang'unika kichini chini afu tukitishiwa tunakaa kimya au kuomba msamaha, kitu ambacho kinampa mwanya Fisadi kuona kuwa kashinda. We have to do something on this...dawa ipo ila cwezi kumwonesha adui silaha zangu. We ngoja tu...
   
 4. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lipuka mwenyewe, hatutaki shari Watanzania.
   
 5. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nikubaliane na wewe kwamba kwa kiasi kikubwa kinachochangia kuendelea kutawalia na wakoloni wazawa ndani ya nchi yetu ni WOGA WA KUTHUBUTU sijui ndo hicho unachokiita nidhamu ya woga? Ndugu zangu kama elimu kwa kweli vyombo husika vimejitahidi sana. Watanzania wa leo, wengi ukiwauliza sababu za uduni wa maisha yao watakuambia kwa asilimia kubwa zinasababishwa na mfumo wa utawala/uongozi wakiwa na maana uongozi bado haujajitoa ipasavyo kutumika kwa maslahi ya umma. Lakini, watajitoaje ili hali hawajui kwa nini twaishi kwa shubiri badala ya asali.
   
 6. L

  Leornado JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hujajua nimemaanisha nini ndugu yangu...Hilo jibu lako linaonyesha jinsi gani ulivyo muoga, hutaki shari wakati TZ ni shari kila mahali coz ya ufisadi???Au we mwenzetu uko system ndio maana unajidai umeridhika?? Usiusemee umma, kama wewe hutaki kupigania haki ya nchi yako tuliza boli. Watanzania wengĂ­ tu maskini na ndio maana we are fighting for our rights.
   
 7. Djunior

  Djunior Member

  #7
  Nov 23, 2010
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndg yangu Leornado, nakupongeza kwa topic yako yenye kuleta ujasiri. Ndg zangu wapenda maendeleo, Wengi wameongea mengi kuhusu Tanzania yetu kuhusu utawala ulioko madarakani, mengi yamesemwa na yanaonekana kwa macho.
  Watu wengi wanateseka ktk nchi hii na hawana mwelekeo ktk maisha yao ya kila siku. Ili mwamini Bw Leornado anasema kweli tuliambiwa mtanzania atapata milo mitatu kwa siku inakuwaje mtanzania anaishi chini ya dollar 1 kwa siku, ndio maana kuna usemi huu WAMETUPIMA VIATU MWAKA HUU NA BAADA YA MIAKA MI5 MTAULIZWA MNA VAA NAMBA NGAPI. Wanzania tujipange tuwe na ujasiri tujikomboe na maliza kwa kuuliza swali. Umekutana na Mamba mtoni kukimbia ni vigumu je utajitoa sadaka kwa kujitupa mtoni au utapambana mpaka tone la mwisho la damu yako?
   
 8. Emasa

  Emasa Member

  #8
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Ni kweli kabisa kama hatutakua wenye kuelewa tunataka nini na kukisimamia tukaendelea na hizi nidhamu za uoga huku tukijua kabisa ni haki yetu kujua kule tunakopelekwa na kuwa na mchango mkubwa wa maamuzi kwa sababu sio siri Serikai imekua ya wachache wasiopendwa ndio wanaotuamulia mambo kwa sababu wana uwezo wa kiuchumi wakitumia mali za Taifa hili kuzidi kujinufaisha na kujiwekea udhatiti madarakani bila kujali mwanachi wa kawaida nasi tupo tu tunawwangalia huku tukiogopa kuchukua hatua zozote kuwaonyesha kuwa hatukubaliani na wanayofanya. Nakubaliana na aliesema kutalipuka siku moja. Kwa sababu sasa this is more than much. Wote wanao waunga mkono hawa jamaa ni Mafisadi wenzao, watoto wao au wananufaika moja kwa moja na uovu wanaofanya so hata kama wanajua ukweli kuwa wanafanya hovyo wanawaunga mkono sababu wanafaidika, Jamani tuamke sidhani kama hatujui mbivu na mbichi ni zipi.
   
 9. Emasa

  Emasa Member

  #9
  Nov 23, 2010
  Joined: Nov 14, 2008
  Messages: 38
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  hakuna kujitoa sadaka mpaka kidole cha mwisho kishindwe kujitikisa ni kukabiliana na kupambana.
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,819
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  wewe ndio walewale mkisikia kulipuka mnafikiri mabomu. si ndiyo
   
Loading...