Serikali ikiwalazimisha wananchi wapige kura, nao wananchi watailazimisha iwaandishe wote walitimiza umri wa kupiga kura. Hao wanaonyimwa kuandishwa wakiandikishwa na kupiga kura, serikali ya ccm lazima idondoke. Mpaka hapo, kipi bora kwa serikali ya ccm?Muda wa kupiga kura huko Misri umeongezwa kufuatia watu wachache kujitokeza kupiga kura. Wananchi ambao bado hawajapiga kura wamehimizwa waende wakapige kura na wasiofanya hivyo watatozwa faini.
Wakati umefika sasa serikali ya Tanzania iige mfano huu wa Misri ili kuwafanya watanzania wajue umuhimu wa kupiga kura. Katika uchaguzi mkuu uliopita 25% ya watu waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura huku 75% wakiingia mitini. Watu wengi hujiandikisha kupiga kura kwa ajili tu ya kupata kadi ya mpigakura ambayo huitumia kama kitambulisho. Watu kama hawa hawatambui kabisa umuhimu wa kupiga kura. Lakini inasikitisha kwamba wakichaguliwa viongozi mafisadi ndio huwa wa kwanza kulalamika.
Serikali iige nchi ya Misri--itunge sheria kali kuwabana wananchi wote wanaojiandikisha wawe wanapiga kura. Mtu akishapiga kura apewe kitambulisho maalum atakachokuwa anakitumia kupata huduma kama vile tiba, elimu, maji, mikopo, nk. Asiyepiga kura anyimwe huduma hizi mpaka uchaguzi ujao. Hii itarejesha nidhamu ya kupenda kupiga.
utaratibu huo hufuatwa na wapenda haki na democrasia tu , serikali hii haiwezi kuhamasisha watu kujitokeza kupiga kura , maana kufanya hivyo ni sawa na kujichimbia kaburi .
Muda wa kupiga kura huko Misri umeongezwa kufuatia watu wachache kujitokeza kupiga kura. Wananchi ambao bado hawajapiga kura wamehimizwa waende wakapige kura na wasiofanya hivyo watatozwa faini.