Wasiopiga kura Misri kutozwa faini

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,216
2,000
Muda wa kupiga kura huko Misri umeongezwa kufuatia watu wachache kujitokeza kupiga kura. Wananchi ambao bado hawajapiga kura wamehimizwa waende wakapige kura na wasiofanya hivyo watatozwa faini.

Wakati umefika sasa serikali ya Tanzania iige mfano huu wa Misri ili kuwafanya watanzania wajue umuhimu wa kupiga kura. Katika uchaguzi mkuu uliopita 25% ya watu waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura huku 75% wakiingia mitini. Watu wengi hujiandikisha kupiga kura kwa ajili tu ya kupata kadi ya mpigakura ambayo huitumia kama kitambulisho. Watu kama hawa hawatambui kabisa umuhimu wa kupiga kura. Lakini inasikitisha kwamba wakichaguliwa viongozi mafisadi ndio huwa wa kwanza kulalamika.

Serikali iige nchi ya Misri--itunge sheria kali kuwabana wananchi wote wanaojiandikisha wawe wanapiga kura. Mtu akishapiga kura apewe kitambulisho maalum atakachokuwa anakitumia kupata huduma kama vile tiba, elimu, maji, mikopo, nk. Asiyepiga kura anyimwe huduma hizi mpaka uchaguzi ujao. Hii itarejesha nidhamu ya kupenda kupiga.
 
isotope

JF-Expert Member
Apr 4, 2012
2,392
0

Serikali ikiwalazimisha wananchi wapige kura, nao wananchi watailazimisha iwaandishe wote walitimiza umri wa kupiga kura. Hao wanaonyimwa kuandishwa wakiandikishwa na kupiga kura, serikali ya ccm lazima idondoke. Mpaka hapo, kipi bora kwa serikali ya ccm?
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,564
2,000
utaratibu huo hufuatwa na wapenda haki na democrasia tu , serikali hii haiwezi kuhamasisha watu kujitokeza kupiga kura , maana kufanya hivyo ni sawa na kujichimbia kaburi .
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,216
2,000
utaratibu huo hufuatwa na wapenda haki na democrasia tu , serikali hii haiwezi kuhamasisha watu kujitokeza kupiga kura , maana kufanya hivyo ni sawa na kujichimbia kaburi .

CCM hutumia udhaifu wa watanzania ujinga wa watanzania kuendelea kukaa madarakani. Wanajua fika kwamba watu wengi wasiojitokeza kupiga kura ni wale waliokata tamaa na ugumu wa maisha pamoja na ukandamizaji wanaofanyiwa na serikali. Ikiwa watawalazimisha kwenda kupiga kura watatumia mwanya huo kuwaondoa madarakani. Hawataki kabisa kuwachokoza watu hao wasije wakawatilia kitumbua mchanga.
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Lusungo

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
21,287
2,000
Hivi kila kitu tuige watu tutakua binadamu wa vipi?

kupiga kura ni uamuzi wa MTU haupaswi kuhojiwa...

usifikiri kila MTU ana muda wa kupoteza kwenye foleni
 
tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,216
2,000
Lusungo, meiga vingapi? ufisadi, uwongo, udokozi, wizi na nini?

Kumbe wanaopiga kura ni wale wenye muda wa kupoteza kwenye foleni?
 
Muk

JF-Expert Member
Sep 4, 2012
551
195
Muda wa kupiga kura huko Misri umeongezwa kufuatia watu wachache kujitokeza kupiga kura. Wananchi ambao bado hawajapiga kura wamehimizwa waende wakapige kura na wasiofanya hivyo watatozwa faini.

Wakati umefika sasa serikali ya Tanzania iige mfano huu wa Misri ili kuwafanya watanzania wajue umuhimu wa kupiga kura. Katika uchaguzi mkuu uliopita 25% ya watu waliojiandikisha walijitokeza kupiga kura huku 75% wakiingia mitini. Watu wengi hujiandikisha kupiga kura kwa ajili tu ya kupata kadi ya mpigakura ambayo huitumia kama kitambulisho. Watu kama hawa hawatambui kabisa umuhimu wa kupiga kura. Lakini inasikitisha kwamba wakichaguliwa viongozi mafisadi ndio huwa wa kwanza kulalamika.

Serikali iige nchi ya Misri--itunge sheria kali kuwabana wananchi wote wanaojiandikisha wawe wanapiga kura. Mtu akishapiga kura apewe kitambulisho maalum atakachokuwa anakitumia kupata huduma kama vile tiba, elimu, maji, mikopo, nk. Asiyepiga kura anyimwe huduma hizi mpaka uchaguzi ujao. Hii itarejesha nidhamu ya kupenda kupiga.

hahaha na huku uje huo utaritibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom