Washkaji wananiogopa,ushauri please!!

The Magnificent

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Posts
2,694
Reaction score
1,250
Heshima kwenu wakuu!!

Hili suala hata mimi binafsi linanishangaz sana....

Ninaishi na rafiki yangu Gheto( kichuo chuo) huu ni mwaka wa tatu sasa

Amekuwa akiniambia kuwa washkaji wananiogopa(hasa majirani,ambao pia ni wanachuo wenzetu)

Yeye huwa ananiambia hata yeye anashangaa kwa nini make inaweza kutokea hata ishu ninayoweza kuulizwa mimi(wakati nipo) nisiulizwe mpaka jamaa arudi,ndipo anaulizwa....(ikiwemo michango kama vile Luku,etc)

Binafsi nilikuwa siamini kama kweli naogopwa,ila juzi hapa.....huyu jamaa angu ambaye naishi nae,kuna jambo alinionge wakiwa na jamaa mwigine(jirani yetu)

sasa ikatokea jamaa(jirani) amekuja gheto na kunikuta nipo na huyu tunaeishi nae pamoja.......bila kuulizwa,kwa woga akaanza kunisimulia jinsi walivyokuwa wanaongea mambo yangu(na jamaa ambaye naishi nae)...

sasa hapa najiuliza..mimi ni anti social kweli? mbona hii imeanza juzi kati? (nilipoanza chuo) na katika kipindi chote cha makuzi yangu nimeishi na watu vizuri in such a way mpaka leo nawasilina nao sana sana....tena wananitafuta wao......hawa wa chuo vipi....?? au huyu jamaa ninayeishi nae ndo snitch nini.....au nina tabia gani inayowafanya waniogope?? mbona napiga nao stori vizuri tu? au .....make hizi taarifa za kuogopwa napewaa sana sana na huyu mdau ninayeishi nae...

Naombeni msaada wa mawazo hapa......make hata siwaelewi elewi.......


 
Kam dawn, we fanya uchunguzi tafuta kadem kakuoshea Lungu halaf katumie kawe kanakuletea Taarifa za kii intelijensia bila ya kujua what is your interest, unajua wapelelezi wenye mahusiano ya kukung'utana huwa wafanisi sana!
 
Sasa wewe ukiletewa taarifa si uulize imetoka wapi na um face alieleta
ili next time akuletee mwenyewe?

labda una pozi za kutotaka kuguswa
 
Kama chuo chenyewe ni IFM wanaweza kuwa na sababu ya msingi ya kukuogopa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kama chuo chenyewe ni IFM wanaweza kuwa na sababu ya msingi ya kukuogopa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Haahaa fafanua mkuu
 
hiyo ni sifa mbaya kwa kijana kama wewe, unabidi ufanye uchunguzi, labda unatabia ya ku-acha watu
 
Itakuwa unaendekeza Mashauzi Mbuzi na Kujiona Hot Cake Sanaaa! Itakuwa uko soo into yourself!Hujiassociate na watu, wataka watu tu ndo wakufate wewe na kukusemesha tu! Inaonesha hapo unapoishi wala hujihangaishi kujiassociate na hao majirani afu utegemee wasikuogope! Mtu unajifanya busy na chuo, ukija ndani, ukitoka chuo! Lazima uogopwe!Itakuwa huyo mwenzio anawasalimia, anachat chat nao kibingwa kuwauliza vipi mitikasi (Not because he cares ila jst being polite!) na kumake nao comversation. Ni kitu kizuri kjuliana hali na majirani! ONGEA NA WATU UVAE VIATU!Mtu akikusemesha once ukajibu briefly atakungojea uanzishe comvrsation ukiignore basi anajikataa mazima! Kuna jirani yangu hapa aliibiwa mchana sababu ya kuendekeza mashauzi wala hawakumpigia simu kama kuna tatizo ama vipi! Majirani usipoelewana nao NUNDA sanaaa!
 
wewe utakuwa n. nyota ya simba, kuchinguze
 
Majibu unayo mwenyewe, hapa unataka ku confirm tu kama ndo hivyo. HUNA TIME NA WENZAKO, UPO KIVYAKO VYAKO. Hii ni tabia mbaya mbele ya jamii. Lara 1 ameshaeleza vizuri tu ktk mchango wake. BADILI TABIA!
 
...unapenda kitu gani...mf. Ni aina gani ya michezo unayopenda?
 
Watu wakikuona wanakukwepa au wanakukimbia???
Ninahisi neno "kuogopwa" limetumika ndivyo sivyo hapa...
 
Watu wakikuona wanakukwepa au wanakukimbia???
Ninahisi neno "kuogopwa" limetumika ndivyo sivyo hapa...

kalitumia sahihi kabisa..

sema kasema ye mwenyewe toka kaingia chuo alikuwa anajifanya yupo busy ndio sababu ya yeye kutemwa kiaina na washkaji wake..
 
1. Wewe ni mtu wa dini sana?
2. Huwa husalimii au kurudisha salamu pindi usalimiwapo?
3. Una mambo ya kishirikina?
4. Umeathirika na tabia kama za ulevi n.k?
5. Umepanga karibu na madada wasioolewa au wasichana/wanawakr wasio na kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…