Washa Brender...!!

kabanga

Platinum Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
37,649
Reaction score
19,042
Siku ya kwanza
MUME: Halooo vipi mke wangu salama weye?.
MKE: Salama tu
MUME: Uko wapi?
MKE: Jamani si niko nyumbani
MUME: Mhh kama kweli uko nyumbani washa brender nisikie.....mke akawasha brender
MKE: Umesikia?
MUME: Okay haya mi natoka kazini naja
Siku ya pili
MUME: Vipi mko salama huko?
MKE: Tupo kama ulivyotuacha
MUME: kwani uko wapi?
MKE: Niko nyumbani napika
MUME: Washa brender kama kweli uko nyumbani
Mke akawasha brender
MKE: Umesikia?
MUME: Poa ntarudi baada ya masaa mawili
Siku sita baadae mume akaamua kurudi bila kumtaarifu mkewe alipofika home kamkuta mdada wa kazi yuko peke yake.
MUME: We mama yako yuko wapi?
MDADA: Sijui ameondoka na brender toka asubuhi
 
ahaa ahaa teh teh mkuu utanivunja mbavu duh hii kali.
 
Kama akiwa kwenye eneo lisilo na umeme itakuwa balaa! labda asingizie umeme umekatika mida hii.
 
Hahahah wanawake sku hz pasu kwa pasu against men

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…