Warsaw yaomboleza kifo cha viongozi wao (Rais, Mkewe, Top Official.......). | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Warsaw yaomboleza kifo cha viongozi wao (Rais, Mkewe, Top Official.......).

Discussion in 'Jamii Photos' started by Steven Sambali, Apr 11, 2010.

 1. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #1
  Apr 11, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Nimepiga baadhi ya picha na nimeamua kuziweka hapa. Hii ya kwanza nimeona nianzie ya Ku-copy maana huko mie sikuwepo na picha zinapigwa na Maro wa hapa ambaye na yeye amekufa. Mpiga picha wa first lady alikosa kiti kwenye ndege na akabaki, ndiyo amebaki hai.

  Pichani, Rais Lech Kaczynski siku alipokea makaratasi ya balozi wetu Ngemera aliyeko German na akiwakilisha pia Tanzania kwa Poland. Picha ya Pili ni Ngemera na Siwa (ubalozi wa Tanzania, German) wakiwa mbele ya President Palace.

  Picha nyingine ntajitahi kesho nikachukue maana leo kulikuwa na watu wengi hadi inaleta uvivu kwenda mbele. Na kibaridi/kimvua kilinikimbiza.
   

  Attached Files:

 2. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #2
  Apr 11, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Umati wa watu mbalimbali waliofika kuja kuwasha mishumaa na kuweka mauwa kwenye President Palace. Pia wengine walikuwa kwenye lile eneo la wazi ambapo kuna kaburi la askari asiyefahamika. Ilinifurahisha na kunishangaza kuwa ingawa watu hawakuambiwa waje, uongozi wa mji wa Warsaw kwa kufahamu kuwa kutakuwa na watu wengi, waliandaa Ambulance nyingi tu, magari ya zima moto, Askari wa City, Polisi, Waokoaji (wamevaa makoti yameandikwa RATOWNIKI) na kali zaidi ni kuweka vyoo (vibanda vimeandikwa TOI TOI).

  Hawa watu wamejiandaa kweli kwa matukio kama haya yakitokea. Na siyo ikitokea ndiyo watu waanze kujiuliza nani atafanya hili au lile.
   

  Attached Files:

 3. Steven Sambali

  Steven Sambali Verified User

  #3
  Apr 13, 2010
  Joined: Jul 31, 2008
  Messages: 314
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Picha zote ziko kwenye huo ukurasa hapo juu.

  Hapa naweka picha moja tu, picha ya mke wa Rais. Huyu mama kama kwenye picha inavyoonyesha, alikuwa ni kama rada inayomuongoza huyu jamaa. Si tu kuwa alihakikisha Mumewe kapendeza ila alikuwa ni msaada mkubwa sana kwa mumewe. Alimtuliza kwenye mambo mengi sana aliyokuwa akifanya. Ingawa mumewe alikuwa ni Profesa wa sheria na Historian mzuri sana, alikuwa akifahamu lugha moja tu, lugha yao. Mkewe alikuwa anaongea Kiingereza, Kifaransa .......... na hivyo kuwa mshauri mzuri sana wa mumewe.
  Nina imani, mafanikio ya mumewe huyu mama alichangia. Nakubaliana na wanaosema, ukipata mke mzuri, basi utafika mbali.
   

  Attached Files:

Loading...