hugochavez
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 1,907
- 1,009
Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.
Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sana. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.
Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?
Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?
Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.
Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babuWarioba ni MKWELI sana, jambo ambalo CCM hawataki.
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
Mbona umeandika unajizungusha na kujikanyaga kanyaga?Warioba Kuchafua hali ya Hewa Bungeni
Wadau, mtu akitonywa jambo ambalo lina maslahi ya kitaifa, ni vema akaliweka hadharani ili kupata tafakuri ya pamoja.
Ni kwamba mdau wangu ambaye yupo kwenye Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo muda si mrefu itamaliza kazi yake, amenitonya kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba atatoa hotuba ambayo kwa maoni yake amesema kuwa huenda ikavuruga maridhiano yanayoendelea Bungeni hivi sasa. Kwamba, Warioba kama sheria ya mabadiliko ya Katiba inavyomtaka, atawasilisha kwenye Bunge Maalum nakala za Rasimu ya Pili ya Katiba. Hii ni baada ya Bunge Maalum kuzinduliwa na Rais Jakaya Kikwete. Mtonyaji amenifahamisha kuwa Warioba atawasilisha Rasimu hiyo siku hiyo hiyo ambayo Rais atalihutubia Bunge. Aidha, mtonyaji amenidokeza kuwa Kabla ya kukabidhi Rasimu hiyo kwa Bunge Maalum, warioba atahutubia Bunge. Sina hakika kama neno kuhutubia ni mahala pake, pengine ingetosha kusema kuwa atasema machache kabla ya kukabidhi.
Wadau, kilichonifanya nije mbio humu jukwaani ni baada ya kusikia dondooo za yale atakayoongea Warioba ambaye siku zote nilikuwa namheshimu kwa kujali maslahi ya taifa ila katika hili, nina hakika hata wadau wengi watamshangaa.
Miongoni mwa atakayosema warioba ni pamoja na haya yafuatayo
Atazungumzia umuhimu wa kura ya Siri kwa wajumbe. Kwamba warioba atatoa maelezo ambayo yana lengo la kuwashawishi wajumbe waunge mkono kura ya Siri. Binafsi sipingi matumizi ya kura hiyo bali hofu yangu ni kuchafuka kwa hali ya hewa. Kama mjuavyo kuwa suala hilo lipo mikononi mwa Kamati ya Maridhiano ambayo imeundwa na Mwenyekiti wa Muda, mzee Kificho. Pia leo tumepata taarifa kuwa zoezi la kufikia muafaka juu ya namna ya kufanya maamuzi Bungeni linaendelea. Sasa huyu Babu Warioba sijui kitu gani kinamshawishi aende kuzungumza jambo hilo Bungeni?
Jambo jingine ambalo Warioba atazungumza ni kuwaeleza wajumbe juu ya umuhimu wa Serikali Tatu. Warioba anataka kulazimisha wajumbe wote waamini kuwa Tume ilikuwa sahihi kupendekeza mfumo wa serikali tatu. Katika hili, pia sina tatizo bali wasiwasi wangu ni namna ya uwasilishaji wake. Ninaamini kuwa wabunge wana akili timamu na hawahitaji mtu kuwasemea uzuri au ubaya wa muundo wa Serikali Tatu. Je wale wanaopendekeza muundo wa serikali moja, mbili, nne na tano nani atawasemea?
Mtonyaji pia amenidokeza kuwa Warioba atatoa hotuba ndefu ambayo itabeba maudhui ya mtazamo wake juu ya mchakato wa Katiba. Binafsi, namshauri Mzee Warioba aangalie upepo unavyoenda. Kwa sasa si wakati wa kushindana. Maridhiano ni jambo muhimu sana. Mwanzo walioanza nao wabunge ni mzuri. Warioba akabidhi tu na asitumie muda mwingi kama ambavyo amepanga kuwachanganya Watanzania na kupandikiza chuki za kuvurugana.
Ni hayo tu wakuu kwa leo. Siku nikitonywa jambo jingine nitakuja fasta kuwatonya.
Mbona umeandika unajizungusha na kujikanyaga kanyaga?
Utaratibu upo hivyo ni lazma atazungumza,
Hali ya hewa ipi itabadilika?
Serikali 3 ipo kwenye rasimu aliyokabiziwa Jk na ushahidi wa video na maandiko ya watannzania wanaopenda serikali tatu.
Mfano baraza la wawakilishi barua ipo
Tatizo lenu ni nini maccm?
naona umevurugwa kweli kweli wewe, au unasemajeUna ufinyu wa fikra kama wabunge wa chama tawala. Kwani serikalu tatu ni dhambi?? Anza zomeazomea kama mluvyo zowea.
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
Mkuu, karika hili suala la Katiba, maridhiano ni jambo la msingi. Si kama anavyofanya huyu babu
warioba anazeeka vibaya kama slaaWarioba wa ajabu sana pale wilayani kwetu bariad wamehoji kata si zaidi ya tano halafu anasema watanzania wengi wametoa maoni yao sijui kayatoa wapi.
Nini kinachotaka kupotoshwa kwa maoni yako wewe pengine unazungumza vitu bila kuwa na uhakika wenye uthibitisho wa kutosha.Tatizo lake babu liko wapi? Yeye atawakilisha mawazo ya wananchi ambayo ccm wanataka kuyapotosha hata kumuona mzee WARIOBA hafai. Tatizo la serikari ya ccm haiutaki ukweli na kamwe hawataweza kusema ukweli mpaka walazimishwe.