je ulimshirikisha toka mwanza kuhusu kutafuta shule na kwamba mwanao akipata nafasi wanaweza kuwasiliana nae??? je huwa mnakutana au kuwasiliana kuhusu maendeleo ya mtoto???
Wapendwa, Salaam poleni na majukumu, tatizo langu ni kwamba nimeachana na mume wangu takribani miaka sita sasa, mtoto wangu wa kawnza ndio alimaliza darasa la saba mwaka huu, katika kuhangaika kumtafutia shule ili ajiunge na kidato cha kwanza nilimchukulia fomu Marian Boys ya Bagamoyo.
Kwenye fomu niliandika jina la baba na namba ya simu kwa kutambua kwamba ni baba wa mtoto, alifanya mtihani na akafaulu, tatizo illilonisikitisha sana ni kitendo cha huyu baba mtu pindi alipopigiwa simu ili atambue hilo aliwajibu kwamba, huyo mtoto yupo kwa mama yake mimi hanihusu hiyo nafasi itoelewe kwa mtu mwingine.
Nilipata maelezo hayo baada ya kupiga simu shuleni ili nijue utaratibu unakuaje na kuambiwa nafasi yake ilishatolewa baada ya baba mtu kuwajibu vile. Je baba kama huyu nimfanyaje kwa hili, mtoto amejua na amekosa amani, naombeni ushauri wenu sijawahi kuumia kama nilivyoumia kwa hili.
Asanteni nakaribisha ushauri wenu
BMP baba amehusishwa na anajiweza kiuchumi sana, tatizo liko ananikomoa na kutafuta kuniumiza kupitia mtoto, ana uwezo mara 100 yanguhakuna kitu kizuri kama mipangilio na mahusiano (kuhusishwa) hata kama mtu hajiwezi kiuchumi ..
hata nikielezea chanzo utasema unataka kusikia kutoka upande wa pili naomba ushauri kwa hili kwanza lililojitokeza
unaelewa nilichokiongea au unaanza tu mashambulizi nimekuudhi na nini, una ona raha mtoto kukosa nafasi ya kusoma kwa ajili ya tu baba ana chuki dhidi ya mama?We ndiye mwenye matatizo, tena nahisi una mapepo ... Umeniudhi sana sio siri.
Mkuu nafikiri ushauri wa hekima na busara unatokana na kusikilizwa kwa pande zote mbili. Bahati mbaya inakuwa vigumu kwa forum kama hii unless huyo ex wako ajitokeze. Kuna mwanaume mmoja alikuja hapa akaeleza matatizo yake dhidi ya mkewe watu wakamwonea huruma. Baadae mke nae akaja hapa kutoa maelezo ya upande wa pili mbona watu waliwithdraw ushauri wao wa mwanzo.
Kama walivyosema wengine the best thing you can do ni to do best for your child. Nenda kwenye shule yenyewe waulize kwa nini hawakukupigia simu wewe? Who knows inawezekana walipiga lakini hukupatikana ndio wakaamua kupiga kwa baba mzazi? Kama hawakupiga then walelezee exactly uhusiano wako na huyo ex na kwa nini amefanya kama alivyofanya.
Lakini kama shule ni ya kidini sana na uliweka contact details za ex wako ili kuleta impression that mnaishi kama familia moja ili mtoto apate nafasi inaweza ku backfire. Pia huwezi kujua ex alisema nini zaidi au aliambiwa nini alipopigiwa simu. Inawezekana kuna kitu aliambiwa na kwa hasira akafikia maamuzi aliyofikia. Siwezi kumhukumu. He is entitled to be heard as well.
Lakini cha msingi ni kumtafutia mtoto shule nyingine unless labda ulikuwa unategemea ex wako amlipie karo. Kama hakupata nafasi hapo shuleni, that is not the end of it. Kwani alifanya mtihani kwenye shule hiyo tuu? Au hakufaulu kwenye shule nyingine alizifanya mitihani?
unaelewa nilichokiongea au unaanza tu mashambulizi nimekuudhi na nini, una ona raha mtoto kukosa nafasi ya kusoma kwa ajili ya tu baba ana chuki dhidi ya mama?
BMP baba amehusishwa na anajiweza kiuchumi sana, tatizo liko ananikomoa na kutafuta kuniumiza kupitia mtoto, ana uwezo mara 100 yangu
wewe liweke wazi tatizo hasa ili uweze kupata ushauri zaidi..
- je ndoa ilikuwaje??
- mliishi kwa muda gani pamoja ???
- nini kilipelekea mtengani
- je alikuwa na upendo na mtoto wakati mnaishi pamoja??
Kyelli .....pole sana but mh unanitisha kuachana miaka sita bado mmewekeana vinyongo?? Sio afya mnajua?Vin D, Baba alikuwa anaelewa kila kitu, hata mtoto alipofaulu nilimweleza, ila nadhani yeye ndio anaamua kumwumiza mwanae kupitia mimi akijua ananikomoa mimi, suala la mtoto kujua alifatilia mwenyewe pale msimbazi na kuambiwa hivyo baada ya kuona mimi namchenga kumwambia ukweli, tatizo hapo sio utoto tunatofautiana uelewa
BPM huyu tumpe mwaliko aje kwenye ofisi zetu bure
BMP baba amehusishwa na anajiweza kiuchumi sana, tatizo liko ananikomoa na kutafuta kuniumiza kupitia mtoto, ana uwezo mara 100 yangu
wewe liweke wazi tatizo hasa ili uweze kupata ushauri zaidi..
- je ndoa ilikuwaje??
- mliishi kwa muda gani pamoja ???
- nini kilipelekea mtengani
- je alikuwa na upendo na mtoto wakati mnaishi pamoja??
mkuu mbona naona hizo information kwa sasa ni irrelevant. Huyo mzee hata kama huyo mtoto asingekuwa amemzaa yeye kiungwana sio vizuri kabisa alichokifanya.
wewe mwanamke utakuwa una matatizo kwa sababu hujitambui na narudia tena inaelekea una stress ile mbaya za maisha kwa sababu kama ulishaachana nae unatoa namba zake za nini ? Ni sawa na ukutane na rafiki yako akuambia naomba namba zako za simu umpe za mmeo alafu umwambie lakini tumeachana Si wehu huo
husn bado zina umuhimu kwani tatizo limejitokea kwa sasa ndo tunaelezwa na bado mtoto ana safari ndefu kielimu naamini kuna mabadiliko yanahitajika ili mtoto atengenezewe njia katika safari yake kimasomo
usilolijua ni sawa na usiku wa giza, alishawahi kuwachukua watoto na kuwapeleka nisikokujua miaka miwili, nilipeleleza nikajua wanakosoma nikaenda ile shule HM akaniambia wale watoto hawana mama yule bwana alimweleza mama yao alishakufa, baadaye watoto walimsumbua alinifuata akanikabidhi watoto hapo ndipo longolongo za matunzo zilipoanzia jamani nina mengi siwezi kusimulia kila kitui