mi kwa kweli ningempongeza kwa kujua ni kidume cha mbegu.....mwanaume asiye na skendo hata moja hafai.....
hahahahaha! Tena bora ameanza kupata maujuzi pembeni asije akatia aibu ndani ya ndoa.
Rudi kwa mchumba wewe.
Tupa kule huyo, mimi natafuta mchumba..au unasemaje!.Heri ya pasaka,kwa kifupi nahitaji msaada wa mawazo,nilikuwa na mchumba mpendwa ktk Bwna kama mimi,na tangu mwanzo tulikubaliana sisi kama wakristo hatutakiwi kufanya tendo la ndoa hadi wkt wa ndoa,hilo lilipita bila kupingwa,na ktk kipindi hicho alisema mwk 2012 angeenda kujitambulisha na kwa bahati baba yake kamjibu hadi arudi nchini december,
Sasa ni hv majuzi niligundua kitu,nilikutana nae maeneo ya mlimani city,wkt nipo nae best yangu akawa amenipigia cm kwmba amekuja dar,cm yangu haikuwa na hela nikaomba yake niitumie kumjibu best,nikajikuta inbox nikapigwa na butwaa kwa kuona msg zinaonesha ametoka kufanya uzinzi siku 2 nyuma.
Niliamua kumuuliza ili aniambie ukweli na alikiri kwmba shetani alimpitia anaomba nimsamehe kwa uzinzi wake,ila nimeshndwa kumsamehe na uchumba nimeuvunja je?wapendwa nipo sahihi?naombeni mawazo yenu!
Mimi ni mkristo na naamini katika utatu mtakatifu lakini nikiri kabisa kwa dunia hii ya leo hii notion ya sex baada ya ndoa ina challenges nyingi.Sitaki kuleta malumbano mengine nje ya hii thread lakini mkuu jiulize maswali kwamba je wakati mnapatana kuhusu kufanya mapenzi kabla ya ndoa wote mlikuwa bikira?Je mli-consider udhaifu wa kibinadamu kati yenu?Ukipata majibu ya maswali hayo naomba give him/her another chance.
Rudi kwa mchumba wewe.
angekuwa mume ningefikiria ila mchumba hapana siwezi,magonjwa mengi sikuhz
mm ningependa kukushauri kuwa uachane naye kwani kama ameshindwa kuwa mwaminifu sasa hv asikudanganye kuwa atakuwa mwamininifu siku nyingine. mtu asipokuwa mwaminifu kwa mambo madogo hawezi kuwa mwaminifu kwa mambo makubwa. Tena huyo siyo Mkristo ni kahaba ambaye amekuja kanisani kuvuna mabinti innocent kama wewe. take care hata Yuda hakuishia kupokea vipande vya fedha tu bali aliendelea akamsaliti Yesu Kristo na kisha akajinyonga
huo ni mtego alioutega shetani ili akikunasa, akuoe, akuambukize magonjwa na uishie kufa kabla ya wakati wako
kumbuka mke/mme mwema hutoka kwa Mungu