Haya wadau jiandae kupaa sasa na muondokane na foleni,sikuhizi barabara hazina maana na matrafiki watakufa njaa
Tukae mkao wa kula, wanasayansi wanazidi kufanya mambo yao, sasa wanatuletea magari yanayopaa a.k.a Flying Cars. Usipate tabu kuunga foleni pale ubungo, wewe washa Engine yako ya ndege kisha ruka mwezini kama njiwa, au siyo!!
Magari hayo bado yanakaguliwa, endapo kila kitu kitakwenda sawa, yataruhusiwa kwenda angani mwaka 2012
Hakyanani hizo ajali huko angani tutapopoana si mchezo. Kama barabarini tu ajali ni za kumwaga, huko angani ambako hakuna hata barabara, taa za kuongozea magari, wala askari wa usalama barabarani, itakuwaje kweli?!