Wanawake wenye hizi tabia mnakera

Vumbi la congo

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
672
Reaction score
985
Wanawake ambao mnajifanya mnawivu kupitiliza mnaboa na wala msijidanganye kuwa ukimuonyesha mwanaume wivu uliopitiliza ndio ataamini kuwa unampenda badala yake utakua kero tu.

Wewe mtu gani ukisika tu sms imeingia kwa mwanaume wako macho yanakutoka unataka akuonyeshe mkiwa mpo faragha simu yake ikiita akiamua kuipotezea ili asikatishe maongezi yenu wewe unahisi ni mchepuko umepiga simu ndio maana hajapokea,,

Ila nyie simu zenu mnaweka pin na wala hamtaki ziguswe mapenzi hamuwezi kazi yenu kuwakosesha wenzenu amani na simu zao mnakera sana tena hasa pale inapogundulika kuwa wivu wako ni wa kinafiki
 
Pole sana ...abiria chunga mzigo wako
 
Piga chini kabisa huyo.
Mpe makavu kama ulivyoandika hapa kwa maana wewe ndio uko naye au wewe ni mario so hasira unaleta huku.
Yeye anaogopa usije ukaharibu ugali wenu.
Yeye nitofauti na wewe .
Maybe yeye ndio anatafutaga hela.
Halafu hataki wewe uwe na wengine usimalizie humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…