Wanawake wanaongoza biashara ya mihadarati

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,687
Polisi kitengo cha kuzuia Dawa za Kulevya nchini, wamekamata dawa za kulevya za aina mbalimbali zenye uzito wa kilo 55,285 katika maeneo tofauti ya nchi tangu Januari hadi Desemba 15, mwaka huu. Watu 6,929 wamenaswa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara hiyo ya madawa ya kulevya, na idadi kubwa ikiwa ni wanawake wenye umri wa kuanzia miaka 25 hadi 40.
Source by Mwananchi Jumatatu 17.
 
mhhh..................hili sasa ni janga!!!!
 
binafsi sina, imani saana na hizo data, zilizotolewa na hao wanaodhibiti madawa hayo, mara zote kama si nyingi, wakubwa hawa walioko ktk maofisi hayo,ili kuonyesha kuwa wanafanya kazi machoni kwa wakubwa akiwemo mh Rais, humpelekea data kama hizo. jiulize vyombo vya habari mara zote wameitwa na wakamataji hawa, na kuonyeshwa madawa hayo, pengine na watuhumiwa, ni mara chache saana wanawake wamehusika ktk matukio yote makubwa ya kukamatwa madawa hayo. lkn ktk kukusanya data zakuwafurahisha wakubwa wao, akiwemo rais ,basi hata mtuhumiwa aliyekamatwa na msokoto wa bhang ataorodheshwa ili data zifurahishe, lkn mahakama kesi nyingi za namna hiyo huzifutilia mbali.maana ndo maana hata mahakama zimejiwekea hata utaratibu wa aina za kesi za kupokea. yaani mahakama ya mwanzo , wilaya na mkoa. wanawake wengi wako kwenye ukamatwaji ule mdogomdogo ambao wengi wao hawakupaswa kuorodheshwa ili kuwa na orodha ndefu ya kina mama.kwani wengi wao ni mateja tu yaliyokamatwa yakiwa yanavuta madawa hayo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…