Wanawake mnakera sana kwa tabia hii

Hata kidot com jamani mmmh

mi nashukuru babyto wangu, yeye akitaka uongee nae, kwanza anatanguliza TAFADHALI NITUMIE M-PESA!!!!

duh! kitu cha arusha ni hatari!
 
Nakumbuka wakati niko chuo kuna mmoja niliwahi kumtukana.... Wakati ndio ilikua awe kitoweo.
Bumu ilikua elfu tano kwa siku....
demu anaomba nimnunulie simu ya nokie E63 kipindi kile ilikua kama laki tatu hivi .... Alinichefua... Nikamtukana nikafuta na number yake kabisa

tatizo kweli....
 
mi nashukuru babyto wangu, yeye akitaka uongee nae, kwanza anatanguliza TAFADHALI NITUMIE M-PESA!!!!

duh! kitu cha arusha ni hatari!
Hahahah ni noooma
 
Wewe nawe unakera kwa kukubali kuwa na wanawake kama hao.

Kama vipi piga chini tafuta anayetaka kuhongwa kikweli, kama gari hivi, au nyumba.

Ili hata kama unalalamika ulalamikie kitu cha ukwee, ukweli /s.

Hahahhahaaaaa nimeipenda hii comment
 
ila mi naona anayefanya hivyo kama vile bado mtoto sanaeee........
NB;uache kutuma vocha za mia5
 

yan bado watu wanabeep.?xtreme zote iz,mmh io ni tabia ya mtu tu kwakwel
 
Wewe ulipokuwa ukimuomba mzazi wako hela ya ada ulikuwa humkeri?

Ukiombwa sana ujue umeonekana unazo, la sivyo atakukimbia muda si mrefu

 

Hehehhhee.....aisee? kwa kweli serikali inatakiwa ifikirie tena kiwango cha mishahara.......yaani vijana wanalalamika balaa. Pole sana kaka.........sisi wengine tukipata anayeridhika na vocha tunashukuru Mola..........maana buku tano mara tatu kwa week sio mbaya hehehehhe.
 
Akikuomba vocha ujue ana watu wa kuongea nao..contact list haupo peke yako!! Sasa unavyotuma 500 inabid tu ubipiwe babuu wee!
 

Hao watoto wadogo, acha ku date vijitoto hata maisha haviyajui,tena hao madenti wa chuo....date wanaojitambua utaona, kila ukipata mshahara swala la kwanza atalokuletea mezani ni namna ya wewe na yeye kufungua vitega uchumi na milango ya kuingiza mi fweza kwa future yenu.
 
teh teh teh......mkuu hawa wanawake wa dizaini hii unawatoa wapi!!!??? Yaani type hii wana njaa kali.
Ndio hapo sasa uelewe anataka kujua kama wewe ndio mwisho wa njaa yake au mbio zinaendelea
 

Mi kuna mtu wangu mmoja alikuwa ananiudhi sana, vocha ya kutosha tu huwa namwachia, karibu elfu tano daily lakini kila akinipigia utasikia "honey I have some few free minutes so they will be up anytime will you call me back??" mwanzo sikuwa namind sana ila siku moja kanipigia tunaongea ishu muhimu simu ikakata nami sikuwa na salio na sehemu niliyokuwepo sikuweza kununua na wakati huo utaratibu wa kukopa haukuwepo, hakunipigia na asubui nilimwekea buku tano kwenye simu, iliniudhi sana na kujiuliza maswali mengi sana amabayo sikupata majibu na sitaki kujua majibu yake. Nilichofanya ni kwamba nampa hela ya vocha, kama anashida akinipigia na hizo free time zake zikiisha sipigi, nitapiga nikiwa nna ishu zangu nataka kuongea basi.
Hivi sasa akili imekaa kichwani kwani kama anashida ananipigia na tunaongea vizuri tuu kwa hela yake. sometime hawa watu ni pasua kichwa tuu.....wanapenda sana vitu rahisi rahisi na mentality yao ni ya ajabu sana kwamba mwanaume ndo atimize gharama zote........kazi kweli kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…