Wanawake mna roho mbaya kama nini, ah!

 
Kimeshaumana huku. Mzee anaendesha uber mwanamke kaondoka. Nasikia hela za kiinua mgongo zote mwanamke alichukua kasepa ulaya. Kutoka boss benki mpaka kuendesha uber!!!
 
Mrejesho
 
Maisha yalisonga wakahama nyumba ya kupanga wakajenga bangalow lao. Dada akataka mtaji afanye biashara ya kwenda china kuchukua bidhaa na kuja kuuza bongo. Baadae mtaji ukatetereka akamshauri mzee astaafu kwa hiari wapate mtaji. Mzee akastaafu akakusanya mafao biashara ya kuingiza bidhaa kutoka china ikaendelea. Ikaanza kusuasua, dada akapata connection marekani (Nadhani kupitia biashara za china), akamshawishi mzee wauze nyumba wapeleke bidhaa marekani (sijui bidhaa gani, mi nilisikia tu wameanza biashara ya marekani). Wakauza nyumba wakasepa zao. Baada ya miezi kadhaa mzee amerudi peke yake, dada kabaki marekani eti kapata kazi kwenye makazi ya kulelea wazee. Mzee akataka kurudi kwenye mji wake alikoachaga familia (Mkewe alisharudi kwao japo ni mtu mzima sana. Kwao ni matajiri) akakuta mwanae kapangisha nyumba kwa mkataba wa miaka mitano na aliyepangishiwa kafanya ukarabati mkubwa ambao mzee hawezi kurudisha hiyo hela kwa sababu amefulia mpaka mwisho (Huyo mtoto aliyepangisha nyumba, mzee alimwacha form two hivi miaka hiyo ila sasa hivi ni mkubwa). Mzee wa watu akarudi kijijini kwao mkoa, amekaa weee akaona hakusomeki, karudi Dar huyo mwanae aliyepangisha nyumba kampa kigari chake (Ractis) mzee afanye uber siku zisonge. Mzee anaendeshA HIYO UBER yeye mwenyewe sasa. Ngoja tuone itakuwaje. Ila wanawake akikukamata vizuri anakumaliza.
 
Asante sana mkuu nimejifunza kitu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…