Wanawake kuweni wakweli

Midazolam

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2020
Posts
807
Reaction score
1,349
Amani iwe nanyi wakuu.

Juzi kipindi natoka kazini mida ya saa nne usiku, nilivyofika maeneo ya majumba sita, wanaokaa Ukonga wanapafahamu hapo.

Nikakutana na dada mmoja muda huo natafuta sehemu ya kutoa pesa kwa m pesa. Nikamuona dada mmoja kila akikutana na mwanaume anamsimamisha alafu hakuna hata anayemsikiliza.

Kwa kuwa mi ni bwana huruma nikawa nimesimama pembeni akanifuata, akaniambia kaka naomba usifikirie vibaya hapa natoka Mombasa, Gongo la mboto nimepungukiwa nauli, akaniambia amemaliza pale uhasibu ila anaenda kwao Charambe Mbagala.

Nikamuone huruma nikampa elfu 6, dada alivyokuwa mzuri na shepu safi akasema hii ni namba yangu chukua umenisaidia Sana, nilivyofika nyumbani kila nikipiga namba haipatikani leo nimekutana naye Kariakoo na kumuuliza anasema siyo yeye nikaenda sehemu moja kwa mbele nikawa nakunywa juice maaneo ya msimbani huwa Wana juice tamu sana yule dada akanifuata ni kweli kaka ni mimi naomba unisamehe, nikasema kuwa na amani naomba nikupe namba yangu nikasema dada wala usijali, nikamkaribisha juice akakaa dakika chache vijana wawili wakamfuata na kuanza kumletea vurugu, ikabidi nisikilizie.

Sikuamini kumbe dada tapeli na kweli ni mwanachuo na bado anasoma na yuko mwaka wa mwisho . Nikamaliza ule ugomvi kirahisi tu.

Nimejifunza mambo mengi sana baada ya kuniambia mwanzo mpaka mwisho,

Nikamuahidi kumsaidia ili amalize chuo kwa furaha na amani kama kumpa tu hela za matumizi, nafahamu hapa duniani tunapita tu.

Tuwe wakweli katika maisha na tusiwahukumu watu.
 
Una uhakika ni mwanafunzi?
Kuwa makini sana.. Wema ajali. Narudia tena wema ajali. Utakuja kuingia kwenye matatzo halafu ukose mtu Wa kukufuta machozi
 
Una uhakika ni mwanafunzi?
Kuwa makini sana.. Wema ajali. Narudia tena wema ajali. Utakuja kuingia kwenye matatzo halafu ukose mtu Wa kukufuta machozi
Niko makini sawa mpaka natoa huu ujumbe nimejiridhisha vya kutosha kabisa,na mpaka chuoni uhasibu,niko makini sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…