Kweli kabisa mkuu. Mimi huwa nazisaka sana, na nikiwa nazo ndo nashuhudia vema uzuri wa mwenza wangu usoni mwake ulonifanya nimuoe, ila zikikata napata tabu sana!
Namuona mtu wa tofauti ambaye sikuwahi kuwaza kuwa angekuwa mwenza wangu. Basi nilipoelewa somo vizuri kabisa nikaamua kila ninapokuwa nazo nazitumia na mzuri mwingine ambae sifahamu ubaya wake.
Nakuwa na amani sana kuliko kuzitumia pesa zangu kinafiki na mtu ambaye huniongezea mateso wakati nipo juu ya mawe. Cha msingi ni ku-cover vizuri mahitaji ya msingi ya familia.
Wanawake wa namna hiyo hawajui kuwa kumdhalilisha mume, huwa wanajitengenezea mwanya wa kukosa mambo mazuri kutoka kwetu.