Wanasiasa acheni kuchochea hasira kwa wananchi

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,197
Reaction score
14,890
Kilasiku mnatoa matamko kwamba Tanzania ni nchi Tajiri na ina rasilimali za kutosha ndio maana majirani na mataifa mengine ulimwenguni yanachochea machafuko hapa nchini.

Mlishawahi kujiuliza ni kwanini mnakopa pesa kila uchwao na mkikosa mikopo mnakuwa na unyonge na kusema tuna hali mbaya?

Kama Tanzania ina utajiri kwanini wananchi wanalalamika hali ngumu?

Kwanini mnaongeza madeni kilasiku kwa mikopo isiyoisha na ilhali nchi ni tajiri?

KUANZIA SASA ACHENI KUSEMA NCHI NI TAJIRI, SEMENI NCHI YETU NI MASKINI ILI KUEPUSHA HASIRA KWA WANANCHI.
 
Wamechanganyikiwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…