ni yupi kati ya mke na mume mara nyingi hubadili tabia na kusababisha ndoa yao kusambaratika?
Mwanaume ndo anabadilika.....
Maana sasa atafyeka wanawake wote ambao alikuwa anawish kuwalala
Atakunywa pombe na kuingia bar zote alizokuwa anatamani kuingia
Atahonga kufidia jinsi alivyokuwa anashindwa kuhonga na kuadhirika
Ataonyesha true color zake..... Ataanza dharau sasa na kumuona mkewe mzee mshamba hana hadhi nae
Ndo maana wanawake siku hizi wanafaka wanaume wenye nazo kuepuka maumivu ha moyo
Hakuna ushahidi wowote katika hayo uliyoandika, ni hisia tu. Wanaume wanaofanikiwa kimapato wengi ni watu wenye nidhamu sana katika matumizi ndo maana wanakutajirika. Hata ndoa zao huzipenda na kuzihudumia ipasavyo. Fanya utafiti kidogo kabla ya kuja ni hii "stereotype" inayosababishwa sana na malalamiko ya wanawake walioshindwa kwenye ndoa zao. Kushindwa kwenye ndoa huwapata wote tu wanawake kwa wanaume. Wanawake hulalamika sana openly wakati wanaume huumia kimya kimya.
wana JF najitokeza kuuliza swali linalonitatanisha.Hivi wanandoa wanapopata mafanikio katika maisha yaani toka ufukara kuwa matajiri ni yupi kati ya mke na mume mara nyingi hubadili tabia na kusababisha ndoa yao kusambaratika?Tabia hizo zinaweza kuwa dharau,majivuno,manyanyaso na nyingine mbaya.Naomba jibu tafadhali.
Kijana,
Inawezekana wewe huna uhakika.....
Ila inawezekan mie nimeandika kutokana na kuyaona mara kadhaa