Aliongeza kuwa mitihani ya taifa kwa kidato cha sita na nne kuanzia mwaka 2012 gharama yake itakuwa Sh. 35,000 kwa kila mwanafunzi.
"Ikumbukwe kuwa gharama hizi ni zile ambazo wazazi na walezi walikuwa wakichangia kati ya mwaka 1999 na 2009 kabla ya serikali haijaamua kusitisha uchangiaji huo," alisema.
Mtihani wa Taifa wa kidato cha pili umekuwa ukigharimiwa na serikali toka ulipoanzishwa mwaka 1984 hadi 1994 ulipositishwa, na mtihani huo ulirejeshwa mwaka 1999 na wazazi walichangia gharama za uendeshaji hadi mwaka 2009 wakati serikali ilipoamua kuugharimia kwa kusitisha ada ya mtihani kwa shule za serikali.
Awali, Serikali iliondoa vikwazo kwa wanafunzi wa kidato cha pili pindi waingiapo kidato cha tatu kwa kuvuka pasipo pingamizi lolote.