Walipiga pia kelele wakati wa Mkapa, Wakapiga wakati wa Kikwete na wameshasahaulika, sasa wanaopiga kelele wakati wa JPM nao watasahaulika

GEE2PATEL

Senior Member
Oct 24, 2018
139
293
Kipindi cha Mkapa alikuwepo mtu mmoja anaogopwa na kila mtu yaan Augustine Lyatonga Mrema, akapiga kelele weee maandamano ya kila wakati weee , kuhamasisha fujo weee, lakin mwisho wake akatulia,

Kipindi hicho cha Mkapa pia akaibuka Profesa Lipumba akapiga kelele weee Ngangari ngangari Cuf Ngangari Vijana Ngangari wakaandamana wakamtukana mzee Mkapa weee, wmisho wa siku kimyaaa

Akaja Kikwete , hapa waliopiga kelele ni wengi , alianza Lipumba akapiga keleleeeee akaja Slaa akapiga keleleeeeee kina Mnyika na kubenea ndo usiseme, lakin sasa wote kimya
MBAYA ZAID WAKIWA KIMYA KUAZNIA MREMA , LIPUMBA, SLAA NA WENGINE WANASALIMU AMRI KWA CCM wanakuwa wapoleeeee hahaha

Kuna jamaa mmoja yuko pale kwa nina Lukaku anapiga kelele sana na mbaya zaidi hajui anatetea nini ni kelele tu, ni kama ng'ombe aliyepangwa kuchinjwa wakamkata kidogo wakamkosa kosa atakimbilia kwa majirani na kila anayekutana naye anamdhuru, mbaya zaid huyu sasa ....... hatari sana
hizi nawaambia ni kelele tu na zitaisha

BY EXTERNAL PAYMENT ACCOUNT BENEFICIARY - GEE2PATEL
 
Leo wavuta bangi watakutukana sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Nchi iongozwe ki democracy ndiyo maendeleo yanapokuwa endelevu. Nchi ikiongozwa na chama kimoja au mawazo ya mtu mmoja lazima ikwame. Hao watu kupiga kelele ni afya kwa nchi. Kwani tabia ya kumtukuza kiongozi au chama ni udhaifu.

Tazama pote duniani nchi zilizopiga hatua ni zile za ki democracy. Ulaya magharibi yote ni democratic countries. Na ndiyo hao tunaowapigia magoti kuomba misaada. Tofauti na nchi za kijamaa zilizong'ang'ania kiongozi moja au chama kimoja, hazina chochote . Zaidi ya maneno matupu ya uzalendo. Na hapa ndipo unapoikuta Tz .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmeanza wataalamu wa matusi na kiwete wenu
Nakuhakikishia na hili sitanii, kabla hujafa rudisha hapa mrejesho kama utakuwa na viungo vyote.
Unatambia uzima unaopewa na Mungu kwa kukashfu madhaifu ya watu (kiwete),?
Nani kakwambia una guarantee ya kuwa mzima mwaka huu wote,!? Upumbavu unaoandika humu na kupewa likes na baadhi ya wanaCCM wapumbavu(maana siyo wote) hauna muda Mungu atakufanya uujutie.

kwani hasiitwe kiwete ,? mtu akiwa mweupe tunasema mweupe, mweusi tunasema mweusi, mfupi tunasema mfupi mjane tunasema mjane, kiwete ni kiwete tu
 
Hakumbuki kuwa Lissu alikuwa mzima wa afya yake !! Ameletewa ulemavu na watu wabinafsi wasiotaka kushindanisha hoja .

Tumshukuru Mungu kwa kila jambo.
Nakuhakikishia na hili sitanii, kabla hujafa rudisha hapa mrejesho kama utakuwa na viungo vyote.
Unatambia uzima unaopewa na Mungu kwa kukashfu madhaifu ya watu (kiwete),?
Nani kakwambia una guarantee ya kuwa mzima mwaka huu wote,!? Upumbavu unaoandika humu na kupewa likes na baadhi ya wanaCCM wapumbavu(maana siyo wote) hauna muda Mungu atakufanya uujutie.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mmoja alipiga kelele kuwa ana uwezo wa kununua korosho zote kwa bei ya shilingi 3600 na kuwa atazibangua hata kwa kutumia mabomu. Naona naye kanyoosha mikon sasa hivi yuko kimya hata hakumbuki kama kuna zao linaitwa korosho
 
Nchi iongozwe ki democracy ndiyo maendeleo yanapokuwa endelevu. Nchi ikiongozwa na chama kimoja au mawazo ya mtu mmoja lazima ikwame. Hao watu kupiga kelele ni afya kwa nchi. Kwani tabia ya kumtukuza kiongozi au chama ni udhaifu.

Tazama pote duniani nchi zilizopiga hatua ni zile za ki democracy. Ulaya magharibi yote ni democratic countries. Na ndiyo hao tunaowapigia magoti kuomba misaada. Tofauti na nchi za kijamaa zilizong'ang'ania kiongozi moja au chama kimoja, hazina chochote . Zaidi ya maneno matupu ya uzalendo. Na hapa ndipo unapoikuta Tz .

Sent using Jamii Forums mobile app
Malawi ni nchi iliyo na democracy ya hali ya juu kwa Africa. Malawi ni Nchi maskini zaidi Africa,ktk top ten inashika no 1 na baadhi ya majarida inaiweka 2 au 3.Tanzania ambayo wewe unasema haina Democracy, ktk nchi Tajiri Africa iko kwenye top ten. Hili swala unalizungumziaje?

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
 
Tunajua mmebaki kuwa wachinjaji, mnajibu nguvu ya hoja kwa magobore! Fikra na maarifa ƴenu mmeyafungamanisha na mitutu, hamuwazi tena kama binadamu wa karne ya 21.
Mda unayoyoma, what wil be your legacƴ!? Maana tunaona kila mahali shagalabagala!
 
kwani hasiitwe kiwete ,? mtu akiwa mweupe tunasema mweupe, mweusi tunasema mweusi, mfupi tunasema mfupi mjane tunasema mjane, kiwete ni kiwete tu

Kuna uzi leo una angazia ka ujinga ka kijana Tanzania. Si haba kuona hili pia la matumizi hata ya kiswahili. Penye 'h' hawapaoni pasipo 'h' wanaongezea wao. Hii ni katika uandishi na hata uzungumzaji.

Sasa mkuu hapo kwenye "hasiitwe" ndiyo kitu gani? Believe me hiyo wala siyo 'typo' bali yale yale ya 'mlegezo'.

Pathetic.
 
Tangu mwaka 1977 mpaka 2019, nayaona mabadiliko makubwa ya kifikra kwa watawaliwa, bahati mbaya sana sioni mabadiliko au juhudi zozote za watawala kwendana na hali halisi. ZUBAENI HAPOHAPO.
 
Back
Top Bottom